JUMBE:CCM TUMEJIPANGA,TUMEWEKA WAGOMBEA SAFI WENYE MAONO YA MAENDELEO

Mjumbe wa Kamati ya Siasa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Mhandisi James Jumbe Wiswa akizungumza leo, Novemba 21, 2024, wakati akizindua kampeni za uchaguzi wa serikali za mitaa katika Kata ya Chamaguha Manispaa ya Shinyanga

Na Mwandishi wetu – Malunde 1 blog

Mjumbe wa Kamati ya Siasa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Mhandisi James Jumbe Wiswa, amewaomba wananchi wa Kata ya Chamaguha kuchagua viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi wa serikali za mitaa, akisema chama hicho kimeleta maendeleo makubwa ambayo yanaonekana kila kona ya mkoa huo na nchi kwa ujumla.

Akizungumza leo, Novemba 21, 2024, katika uzinduzi wa kampeni za uchaguzi wa serikali za mitaa katika Kata ya Chamaguha Manispaa ya Shinyanga, ulioambatana na shamrashamra za hapa na pale,  Mhandisi Jumbe amesema CCM imejipanga vizuri na imeleta wagombea safi ambao wanayo dhamira ya dhati ya kutekeleza ahadi za maendeleo kwa kushirikiana na Rais Samia Suluhu Hassan, madiwani na wabunge wa CCM.

“Wananchi wa Chamaguha, nataka niwahakikishie kwamba CCM imeleta wagombea safi, watu wenye maono na nia ya dhati ya kuleta mabadiliko. Tunahitaji viongozi watakaoshirikiana na Madiwani, Wabunge na Rais Samia katika kuleta maendeleo ya kweli. Hawa viongozi wapo tayari kuwatumikia na kuleta maendeleo makubwa katika kata yetu,” amesema Mhandisi Jumbe kwa msisitizo.

Akiwaomba wananchi wachague wagombea wa CCM, Mhandisi Jumbe amefafanua kuwa maendeleo makubwa yaliyofikiwa Shinyanga, kama vile kuboreka kwa huduma za afya, elimu, miundombinu ya barabara na maji, ni matokeo ya usimamizi mzuri wa CCM. 

Mjumbe wa Kamati ya Siasa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Mhandisi James Jumbe Wiswa (kushoto) akiwanadi wagombea wa CCM.

Amesema zawadi pekee ya kumlipa Rais Dkt. Samia  Suluhu Hassan (Mwenyekiti wa CCM Taifa) kwa jitihada zake ni kuwachagua viongozi wa CCM ili kuendeleza maendeleo hayo.

“Rais  Dkt. Samia amefanya makubwa hapa Shinyanga, na zawadi yetu kwake ni kupigia kura wagombea wa CCM. Tunataka kuendelea kushuhudia nguvu na umoja wa viongozi wa CCM katika kuleta maendeleo kwa wananchi,” amesisitiza Mhandisi Jumbe.

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga, Ramadhani Masumbuko, amesema mafanikio makubwa yamepatikana chini ya uongozi wa CCM katika sekta mbalimbali, akitaja baadhi ya mafanikio haya kuwa ni ujenzi wa barabara bora, huduma za afya bora, na utoaji wa maji safi na salama.

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Ramadhan Masumbuko ambaye ni Diwani wa kata ya Chamaguha

 Masumbuko ambaye ni Diwani wa kata ya Chamaguha amewataka wananchi wa Chamaguha kuhakikisha wanachagua viongozi wa CCM ili kuendelea kupata huduma bora na maendeleo endelevu.

“CCM imeleta mabadiliko ya kweli, na tunahitaji kuendelea na maendeleo haya. Hakuna haja ya kufanya majaribio na wapinzani, tumekuwa na mafanikio na tunataka kuyapata zaidi,” amesema Meya Masumbuko.

Wagombea wa CCM, wakiwemo mgombea uenyekiti wa Mtaa wa Sanjo, Moshi Ramadhani,  Mtaa wa Chamaguha, Hussen Matamba; na Mtaa wa Tanesco, Suleiman Mzee Suleiman, wameahidi kuwatumikia wananchi kwa juhudi zote na kuhakikisha kuwa kila changamoto inapata ufumbuzi. 

Wamesisitiza kuwa watajitahidi kufanya kazi usiku na mchana kuleta maendeleo zaidi kwa jamii.

“Tunaahidi kufanya kazi kwa bidii, kuhakikisha tunatatua changamoto zote za wananchi, na kuleta maendeleo yanayostahili. Tutashirikiana na viongozi wa ngazi zote kuleta mabadiliko bora,” amesema Suleiman mgombea Mtaa wa Tanesco.

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utafanyika Novemba 27, 2024.

Mjumbe wa Kamati ya Siasa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Mhandisi James Jumbe Wiswa akizungumza leo, Novemba 21, 2024, wakati akizindua kampeni za uchaguzi wa serikali za mitaa katika Kata ya Chamaguha Manispaa ya Shinyanga – Picha Malunde Media

Mjumbe wa Kamati ya Siasa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Mhandisi James Jumbe Wiswa akizungumza leo, Novemba 21, 2024, wakati akizindua kampeni za uchaguzi wa serikali za mitaa katika Kata ya Chamaguha Manispaa ya Shinyanga

Mjumbe wa Kamati ya Siasa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Mhandisi James Jumbe Wiswa akizungumza leo, Novemba 21, 2024, wakati akizindua kampeni za uchaguzi wa serikali za mitaa katika Kata ya Chamaguha Manispaa ya Shinyanga

Mjumbe wa Kamati ya Siasa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Mhandisi James Jumbe Wiswa akizungumza leo, Novemba 21, 2024, wakati akizindua kampeni za uchaguzi wa serikali za mitaa katika Kata ya Chamaguha Manispaa ya Shinyanga

Mjumbe wa Kamati ya Siasa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Mhandisi James Jumbe Wiswa (kushoto) akiwanadi wagombea wa CCM wakati akizindua kampeni za uchaguzi wa serikali za mitaa katika Kata ya Chamaguha Manispaa ya Shinyanga

Mjumbe wa Kamati ya Siasa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Mhandisi James Jumbe Wiswa akiwanadi wagombea wa CCM wakati akizindua kampeni za uchaguzi wa serikali za mitaa katika Kata ya Chamaguha Manispaa ya Shinyanga

Mjumbe wa Kamati ya Siasa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Mhandisi James Jumbe Wiswa (kulia) akiteta jambo na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Ramadhan Masumbuko ambaye ni Diwani wa kata ya Chamaguha wakati wa uzinduzi kampeni za uchaguzi wa serikali za mitaa katika Kata ya Chamaguha Manispaa ya Shinyanga

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Ramadhan Masumbuko ambaye ni Diwani wa kata ya Chamaguha akizungumza wakati wa uzinduzi kampeni za uchaguzi wa serikali za mitaa katika Kata ya Chamaguha Manispaa ya Shinyanga

Related Posts