RC MACHA AONGOZA MAHAFALI YA 43 WANACHUO HATUA YA PILI VETA SHINYANGA

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Anamringi Macha, akizungumza wakati wa mahafali ya 43 ya Wanachuo wa Hatua ya Pili (Level Two) katika Chuo cha VETA Shinyanga

Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog

 

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Anamringi Macha, ameongoza mahafali ya 43 ya Wanachuo wa Hatua ya Pili (Level Two) katika Chuo cha Ufundi Stadi Shinyanga (VETA), ambapo jumla ya wanachuo 198  kati yao wa kike 55, wa kiume 143 wamehitimu mafunzo katika fani mbalimbali.

 

 Akizungumza kwenye hafla hiyo iliyofanyika leo, Ijumaa, Novemba 22, 2024, Mhe. Macha amewapongeza wanachuo kwa kumaliza mafunzo yao na kuwaonya kutumia elimu waliyoipata kwa malengo ya kuboresha maisha yao na jamii kwa ujumla.

 

“Serikali ipo kuhakikisha mnatoboa maisha, mabadiliko haya ni yenu. Nendeni mkachape kazi, mkawe waungwana na wavumilivu. Mkachangamkie fursa zilizopo mtaani,” amesisitiza Mhe. Macha, akiwashauri vijana hao kujitahidi kutumia elimu yao kwa usahihi ili kuboresha maisha yao na jamii. 

 

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Anamringi Macha

 

 

Ameongeza kuwa mikopo inapatikana kwa urahisi kupitia halmashauri na kwamba wanafunzi hao wanatarajiwa kuelekezwa namna ya kupata mikopo isiyo na riba kwa ajili ya kuanzisha biashara au kujiajiri.

 

Amesema serikali iko tayari kusaidia na kutoa mikopo isiyokuwa na riba kwa vijana, wanawake na makundi maalum ili waweze kuanzisha na kuendeleza miradi ya maendeleo.

 

Aidha, Mhe. Macha ametilia mkazo umuhimu wa vyuo vya ufundi stadi, akisema Rais Samia Suluhu Hassan amedhamiria kuboresha vyuo vya VETA nchini na kwamba serikali inaendelea kutenga fedha kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya vyuo vya VETA, ikiwemo ujenzi wa uzio wa chuo hicho unaotarajiwa kugharimu kiasi cha shilingi milioni 400. 

 

Mhe. Macha pia ameipongeza VETA kwa kuanzisha mfumo wa kupika kwa gesi badala ya kutumia mkaa, akisema ni hatua nzuri katika kupunguza athari za mazingira. 

Wahitimu wa Elimu ya Mafunzo ya Ufundi Stadi Daraja la Pili (II) wakicheza muziki

 

Ameeleza kuwa vijana wanapaswa kubadilika na kuzingatia mifumo bora katika kufanya kazi, akionya kuhusu matumizi mabaya ya vyombo vya moto na usafiri, akitoa mfano wa baadhi ya waendesha bodaboda kutokufuata taratibu na kuweka watoto kwenye tenki la mafuta, jambo alilolielezea kuwa siyo salama.

 

Mhe. Macha amesisitiza kuwa waendesha bodaboda wanapaswa kupata mafunzo rasmi ya udereva ili kudhibiti pia ajali za barabarani.

 

“Pia Tutahakikisha waendesha bodaboda wanakuja hapa VETA kujifunza masuala ya udereva, wale wote ambao hawajapata mafunzo waje hapa VETA. Kuna baadhi ya bodaboda hawana utu. Bodaboda wanabeba watu wengi,mbele anakalishwa mbele kwenye tenki la mafuta, siyo jambo zuri. Ubebaji tu wa mishikaki ni kosa, bado mnaweka mtoto kwenye tenki mnamkaanga, mnaanza kuwafanya watoto kuwa magarasha wakiwa utotoni. 

 

Tuache kuwaweka watoto kwenye matenki, pamoja na kwamba inaonekana kama vyombo vya usalama vinafumbia macho mishikaki lakini hili la kuweka watoto kwenye mishikaki halipaswi kufumbiwa macho”,amesisitiza Mhe. Macha.

 

 

Katika sehemu nyingine, Mhe. Macha amezungumzia umuhimu wa VETA kama kiungo muhimu katika ujenzi wa taifa, akisema vyuo vya ufundi stadi vinachangia pakubwa katika kutoa wataalamu waliobobea katika fani mbalimbali, akiwemo umeme, ujenzi, na uchakataji wa madini. 

 

Kwa upande wake, Mkuu wa Chuo cha VETA Shinyanga Mwl. Abraham Richard Mbughuni amesema idadi ya wanafunzi waliodahiliwa katika kozi za muda mrefu kwa sasa ni 525 na kozi fupi ni 753 kwa kipindi cha kuanzia mwezi Julai 2024 hadi Novemba 2024.

 

“Tunapenda kumshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa jinsi anavyoendelea kuiangalia Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi nchini kama kiini cha kuleta mageuzi ya kweli ya uchumi nchini kupitia VETA yenye dhamana ya kuiandaa nguvu kazi yenye ujuzi”,ameongeza Mwl. Mbughuni. 

 

Mkuu wa Chuo cha VETA Shinyanga Mwl. Abraham Richard Mbughuni 

 

 

Amesema ili kukabiliana na gharama za ujenzi zinazopanda kila siku, chuo cha VETA Shinyanga kimeanza kuwafundisha vijana ufyatuaji wa tofali zinazoingiliana (Interlocking bricks) kwa ajili ya ujenzi wa nyumba zenye gharama nafuu.

 

“Mafunzo haya yatakuwa ni msaada mkubwa kwa vijana wetu kwani mara watakapohitimu yatawezesha kujiajiri na kuleta mapinduzi ya ujenzi wa nyumba zenye gharama nafuu katika maeneo yao nan chi kwa ujumla”,amesema Mwl. Mbughuni.

 

“Pamoja na mitambo na vifaa vilivyoko katika chuo chetu, pia tuna mashine mbili za kipekee ambazo ni Surface Grinding machine ambapo mashine hiyo ina uwezo mkubwa wa kusawazisha ‘cylinder heads’ za magari ya aina zote mara zinapopatwa na hitilafu ‘leakages’ kwa muda mfupi sana (wastani saa moja) ikilinganishwa na ‘Milling machine’ inayofanya kazi za aina hiyo kwa zaidi ya saa saba”,ameeleza.

 

Amesema Mashine nyingine ni ‘Computerized Numerical Control (CNC) Machine ambayo ina uwezo wa kuchora maumbo mbalimbali na kuandika maandishi ya aina tofauti kwenye madini, mawe, chuma, mbao, vibao vya mawe ya msingi, utambulisho wa ofisi katika majengo ya umma na kadhalika.

 

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Anamringi Macha akizungumza wakati akishuhudia mitambo ya kisasa na adimu iliyopo katika Karakana ya Ukataji Madini Vito katika Chuo cha VETA Shinyanga.

 

 

“Mashine hizi ni kati ya mashine za kisasa na adimu katika maeneo mbalimbali nchini na hupelekea wananchi kutumia gharama kubwa kufuata huduma hizo Dar es salaam na kwingineko. Hivyo tunapenda kuujulisha umma kuwa huduma hizi zinapatikana katika Chuo cha VETA Shinyanga kwa gharama nafuu”,ameongeza Mwl. Mbughuni.

 

Amezitaja changamoto wanazokabiliana nazo ikiwemo kukosekana kwa uzio wa Chuo ambapo sasa zinahitajika shilingi  milioni 405 ili kukamilisha ujenzi huo huku akiitaja changamoto nyingine kuwa ni uchakavu na uchache wa magari ya kujifunzia udereva wa awali (basic driving cars) magari ya abiria (PSV), magari ya mizigo (heavy duty vehicles) na mitambo (grader, excavator, wheel loader, folklift, roller n.k).

 

ANGALIA PICHA HAPA CHINI

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Anamringi Macha, akizungumza wakati wa mahafali ya 43 ya Wanachuo wa Mwaka wa Pili (Level Two) katika Chuo cha Ufundi Stadi Shinyanga (VETA) leo Ijumaa Novemba 22,2024- Picha na Kadama Malunde – Malunde 1 blog

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Anamringi Macha, akizungumza wakati wa mahafali ya 43 ya Wanachuo wa Mwaka wa Pili (Level Two) katika Chuo cha Ufundi Stadi Shinyanga (VETA)

 

Wahitimu wa Elimu ya Mafunzo ya Ufundi Stadi Daraja la Pili (II) wakiwasili ukumbiniWahitimu wa Elimu ya Mafunzo ya Ufundi Stadi Daraja la Pili (II) wakiwasili ukumbini
Wahitimu wa Elimu ya Mafunzo ya Ufundi Stadi Daraja la Pili (II) wakicheza muziki

Wahitimu wa Elimu ya Mafunzo ya Ufundi Stadi Daraja la Pili (II) wakicheza muziki

 

Mkurugenzi wa VETA Kanda ya Magharibi, Asanterabi Kanza akizungumza wakati wa mahafali ya 43 ya Wanachuo wa Hatua ya Pili (Level Two) katika Chuo cha VETA Shinyanga

Mkuu wa Chuo cha VETA Shinyanga Mwl. Abraham Richard Mbughuni akizungumza wakati wa mahafali ya 43 ya Wanachuo wa Hatua ya Pili (Level Two) katika Chuo cha VETA Shinyanga

Mratibu wa Mafunzo VETA Shinyanga, Rashid Hamis Ntahigiye akizungumza wakati wa mahafali ya 43 ya Wanachuo wa Hatua ya Pili (Level Two) katika Chuo cha VETA Shinyanga

Mhitimu Isaya Stephano akisoma risalawakati wa mahafali ya 43 ya Wanachuo wa Hatua ya Pili (Level Two) katika Chuo cha VETA Shinyanga

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Anamringi Macha (katikati) akiwa katika Karakana ya Ukataji Madini Vito katika Chuo cha VETA Shinyanga.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Anamringi Macha (aliyevaa miwani kushoto) akiwa katika Karakana ya Ukataji Madini Vito katika Chuo cha VETA Shinyanga.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Anamringi Macha akiwa katika Karakana ya Umeme katika Chuo cha VETA Shinyanga

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Anamringi Macha akiwa katika Karakana ya Ujenzi katika Chuo cha VETA Shinyanga

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Anamringi Macha akikabidhi cheti kwa mmoja wa Wahitimu wa Elimu ya Mafunzo ya Ufundi Stadi Daraja la pili (II) katika chuo cha VETA Shinyanga

Related Posts