Mkuu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Benki ya CRDB, Emmanuel Kiondo akizungumza jijini Dar es Salaam wakati wa hafla fupi iliyowakutanisha wadau mbalimbali wa muziki kwa lengo la kujadili masuala tofauti tofauti yanayohusiana na muzikin katika hafla iliyoandaliwa na Mdundo.Com.Mkurugenzi Mkazi-Tanzania wa Mdundo.com, Maureen Njeri akizungumza jijini Dar es Salaam wakati wa hafla fupi iliyowakutanisha wadau mbalimbali wa muziki kwa lengo la kujadili masuala tofauti tofauti yanayohusiana na muzikin katika hafla iliyoandaliwa na Mdundo.Com.
MKUU Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Benki ya CRDB, Emmanuel Kiondo, amesema kuwa Wasanii wa Muziki nchini wanahitaji elimu ya uwekezaji ili iwasaidie kutumia vizuri vipato vyao vinavyotokana na kazi zao hasa pale wanafikia mwisho wa kazi hizo.
Akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam Novemba 21, 2024 wakati wa hafla iliyowakutanisha wadau mbalimbali wa muziki kwa lengo la kujadili masuala tofauti tofauti yanayohusiana na muzikin iliyoandaliwa na Mdundo.Com. Amesema kuwa Amesema kuwa pia wanatakiwa kupata elimu ya namna ya kutumia mifumo ya kidijitali kusambaza maudhui yao.
Amesema ipo mifano ya wasanii wakubwai ambao walifanikiwa kupata fedha nyingi kupitia kazi hiyo lakini baadae wanarudi kuwa masikini baada ya kukumbwa changamoto mbalimbali.
“Na hii yote inatokana na kukosekana kwa elimu ya fedha, kwamba msanii anakuwa na wakati mzuri, anafanya kazi na kutengeneza fedha lakini badala ya kuwekeza, anatumia vibaya na mwisho wa siku anapokuja kupoteza uwezo wake wa kufanya shughuli yake hiyo anakufa masikini.” Amesema
Kwa upande wa Mkurugenzi Mkazi-Tanzania wa Mdundo.com, Maureen Njeri wakati wa hafla amesema Mdundo ina watumiaji hai milioni 37.8 kila mwezi na watumiaji milioni 3.1 kwa mwezi nchini Tanzania na kwamba zaidi ya wasanii 24,000 wa Tanzania wamefungua akaunti kwenye jukwaa na wanatengeneza hela kutoka Mdundo.
Ameeleza kuwa wanafanya kazi chapa za kampuni mbalimbali kwa lengo la biashara chapa hizo ni kama Vodacom Tanzania, Castal lite na pia wapo kwenye kampeni ya VYB, hii inadhihirisha audio solutions zinazotolewa na Mdundo na jinsi zinavyoweza kubadilishwa kulingana na hadhira iliyopo.
Amesema kuwa wanakampeni inayolenga vijana wa Kitanzania wenye umri kati ya miaka 15 na 28, ili waweze kufikia mtindo wa maisha wa kidijitali.
Moureen amesema kuwa wanajivunia kuwa jukwaa la kwanza la Muziki Tanzania kuwaleta pamoja wadau wa tasnia ya mziki ili kushiriki katika masuala mbalimbali
Licha ya hayo amesisitiza kuwa Mdundo Tanzania inajukwaa kubwa la wasanii ambalo ni linafursa nyingi za kushirikishana ikiwemo kutangaza muziki wa msanii hasa wakati wa kuzindua albamu, kutoa wimbo mpya na kutangaza chapa mpya.
Kwa upande wa mdau wa muziki, Aman Martin, amesema kuwa kuna haja ya kuongeza uelewa kwa wasanii wa mziki na wanaowasimamia ili wafahamu namna ya kutumia vizuri mifumo ya kidijitali katika kusambaza kazi zao. Pia kutokujua namna sahihi ya kutumia mifumo ya kidijitali katika kusambaza maudhui kwa wasanii wengi na kwamba na kazi kubwa ya kufanya kuhakikisha wana kuwa na taarifa na maarifa ya kutosha ili iwasaidie kuepukana na changamoto za kufanya kazi isiyo na manufaa.
‘Bila kujali ni maarufu au laa, msanii akitumia vizuri mifumo ya kidijitali kusambaza maudhui ya kazi yake, ni rahisi kunufaika, cha msingi ni wanamuziki hao kufahamu namna mifumo hiyo ya kidijitali inavyoendeshwa na namna ya kuitumia katika kuinua au kutangaza kazi zao. “Amesema Martin.