WAGOMBEA WA UPINZANI HAWANA ILANI WALA MIPANGO MSIPOTEZE MUDA

 CPA MAKALLA: MSIWACHAGUE 

Na Mwandishi Wetu.

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimewaomba Watanzania kutopoteza muda wao kwa kuwachagua wagombea wa vyama vya upinzani katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwani hawana mipango ,malengo na Ilani wanayoweza kuitumia katika kuleta Maendeleo na badala yake wahakikishie wanachagua wagombea wa CCM.

Ombi hilo limetolewa leo na Katibu wa Halmashauri Kuu(NEC)ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)Itikadi, Uenezi  na Mafunzo CPA Amoss Makalla alipokuwa akizungumza katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika Jimbo la Kawe mkoani Dar es Salaam ikiwa ni muendelezo wa mikutano yake ya kampeni katika Mkoa huo.

CPA Makalla amesema Chama hicho katika kutambua umuhimu wa uchaguzi huo kimefanya uteuzi wa wagombea wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji ambao wanasifa za uongozi na wako tayari kuwatumikia wananchi katika mitaa yao.

Ameongeza kuwa wagombea wa CCM wanepitishwa katika vikao vya Chama na kuchukujwa kwa sifa zao lakini ni wagombea ambao watakapoteuliwa watashirikiana na madiwani, Wabunge na Rais katika kuendelea kuleta maendeleo.

“Wagombea etu wakichaguliwa watakwenda kushirikiana na Madiwani na Wabunge waliopo katika kushiriki kuleta maendeleo lakini wagombea wa upinzani hata wakishinda hawana wa kushirikiana nao wapo kama yatima tu.Chagueni wagombea wa CCM maana wote wanasifa na wako tayari kuleta maendeleo ya nchi yetu.”

Akielezea zaidi amesema wagombea wa upinzani hawana Ilani bali wenyewe wameambiwa na viongozi wao wabuni tu Ilani kutoka kichwani lakini wagombea wa CCM wanayo Ilani ya Uchaguzi lakini wakati huo huo wamepewa na tamko ambalo linatoa maelekezo ya Yale ambayo wanatakiwa kuyatekeleza baada ya kuchaguliwa.

Kuhusu wagombea ambao hawakupata nafasi katika mchakato wa ndani ya Chama amesema Chama hicho kilishafanya vikao nchi nzima na wameyazumza na sasa wapo katika uchaguzi huo wakiwa wamoja na wanauhakika wa kushinda kwa kishindo.

“Baada ya kumaliza mchakato wa ndani wa kupata wagombea tulishafanya vikao na sasa wote tuko wamoja.CCM hakuna kukatwa ila unaweza usiwe umeteuliwa .Hata mimi nilikuwa kugombea ubunge nikashinda lakini sikuteuliwa.

“Ingekuwa CCM wamenikata nisengekuwa Mkuu wa Mkoa na baadae Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama chetu.Hata Abbas Mtevu alishinda Ubunge Temeke lakini hakuteuliwa lakini leo ndio Mwenyekiti  Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam,”amesema.

Amesema kuwa vyama vya upinzani walikuwa wanasubiria ambao hawakupitishwa na Chama kugombea wawachukue lakini wamekwaa kisiki maana wote waliogombea lakini hawakuteuliwa wanaendelea na kampeni za uchaguzi huo.

“Walikuwa wanawasubiri waliokatwa wawachukue lakini wameshindwa.Hata mimi wakati ule sikuteuliwa lakini niliendelea na shughuli zangu nikashiriki kampeni baadae nikateuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa.Nchi nzima Wana CCM tumekubaliana kuwa kitu kimoja na  ushindi wetu uko hadhahiri lakini tunataka kupata ushindi wa kishindo.”


Related Posts