OfisaTarafa wa Nyaishozi Kelvin Berege amekabidhi Reflectors kwa maofisa Usafirishaji ( Boda Boda ) wa Kata zote ndani ya tarafa hiyo.
Lengo ni kuendelea kutoa elimu na kuhamasisha makundi mbalimbali ndani ya jamii, juu ya haki na wajibu wa mwananchi Kupiga/Kupigiwa Kura ifikapo Novemba 27 mwaka huu ambapo utafanyika uchaguzi wa Serikali za Mitaa.