Leo Jumapili, Novemba 2 4, 2024 ni mahafali ya 23 ya Chuo Kikuu cha Mzumbe, Mkoa wa Morogoro.
Katika mahafali hayo yatakayofanyikia chuoni hapo,
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan atatunukiwa Shahada ya Udaktari wa Heshima katika Uongozi ya Chuo Kikuu Mzumbe.
Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa William Mwegoha amesema hiyo itakuwa shahada ya kwanza ya heshima kutolewa na chuo hicho tangu kuanzishwa kwake.
Shahada hiyo ya udaktari wa heshima itakuwa ya tano Rais Samia kuoewa tangu alipoingia madarakani Machi 19, 2021 akichukua kijiti cha mtangulizi wake, hayati John Magufuli aliyefariki dunia Machi 17, 2021.
Shahada nyingine nne ametunukiwa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Tanzania), Chuo Kikuu cha Zanzibar, Chuo Kikuu cha Jawaharlal Nehru (India) na Chuo Kikuu cha Ankara nchini Uturuki.
Aidha, Profesa Mwegoha amesema suala la usawa wa kijinsia limepiga hatua chuoni hapo akitolea mfano, wahitimu wa mwaka huu,”ni karibu 50/50 kwani asilimia 50.2 ya wahitimu ni wanaume na asilimia 49.7 ni wanawake. Naweza kuona jinsi tunavyopiga hatua kwa vitendo.”