UTAPENDA ALIYOYASEMA MBUNGE WA UKONGA MBELE YA MAKALLA WAKATI WA KAMPENI UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA

 

Na Said Mwishehe, Michuzi TV

WAKATI Katibu wa Halmashauri Kuu NEC ya Chama Cha Mapinduzi CCM Itikadi, Uenezi na Mafunzo CPA Amoss Makalla akiendelea na kampeni za uchaguzi wa Serikali za Mitaa Mbunge wa Jimbo la Ukonda jijini Dar es Salaam Jerry Silaa amesema kwa maendeleo yaliyofanywa na Serikali ushindi mkubwa unakwenda kwa wagombea wa CCM.

Akizungumza leo Novemba 24,2024 katika mkutano Jimbo la Ukonga ikiwa ni muendelezo wa mikutano ya kampeni ya CPA Makalla katika Mkoa wa Dar es Salaam,Silaa amesema Jimbo la Ukonga lina Mitaa 70 na Kata 13 lakini kila Mtaa,kila Kata kuna maendeleo makubwa yamefanywa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwani amepeleka fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo.

“Kwa mambo ambayo yamefanywa na Rais Samia katika Jimbo la Ukonga ni makubwa haijapata kutokea .Wakati tunaelekea katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa Novemba 27 mwaka huu tayari katika Mitaa 28 wapinzani wametia mpira kwapani lakini kwa mujibu wa sheria mpya tunasubiria tu siku ya Uchaguzi wapigiwe kura ya ndio.”

Akielezea zaidi katika mkutano huo,Silaa amemwambia CPA Makalla na viongozi wengine wa Mkoa wa Dar es Salaam kuwa wagombea wao watakwenda kueleza mambo mawili kwa wananchi na jambo la kwanza ni kwenda kueleza kuwa yuko jemedari Rais Samia na hakuna wanachomdai ila Rais ndio anawadai na watamlipa kwa kura.

“Katika sehebu zetu Wana Ukonga hakuna tunachomdai Rais DK.Samia  ila yeye ndio tunamdai.Ametufanya mambo makubwa sana kuanzia katika elimu,afya, miundombinu,maji na huduma zote muhimu.Katika elimu ndani ya Jimbo la Ukonga hakuna eneo lenye uhaba madarasa,madawati au matundu ya vyoo.

Madarasa ya Dk.Samia utadhani hoteli za kitalii,”amesema Silaa.

Ameongeza katika eneo la afya ,Rais Samia wakati anaingia madarakani vituo vya afya vinahesabika lakini kwa sasa Tanzania ujenzi wa vituo vya afya umefanyika kila mahali na katika Hospitali ya Kivule huduma zimeimarishwa na dawa na vifaa tiba vya kisasa vipo katika hospitali hiyo 

“Rais ameleta fedha kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu mbinu ya afya sambamba na kuleta fedha za vifaa tiba vya kisasa.Maji yamesambaa katika maeneo mbalimbali ya Ukonga. Jumla ya kilometa 112 za maji yatasambazwa,”amesema.

Pia amesema Jimbo la  Ukonga watu wake wanafanyashughuli mbalimbali ambazo zinawafanya wawe wanatoka kwenda Mjini na kurudi majumbani.

“Tayari Rais DK.Samia Suluhu Hassan ameshasaini mkataba na benki ya Dunia kwa ajili ya mradi wa DMDP na Ukonga tunakwenda kujenga barabara za lami kilometa 72.”

Ameongeza kuwa TARURA nayo inaendelea na ujenzi wa barabara za lami zenye urefu wa nusu kilometa na kilometa Moja katika kila mahali katika barabara zetu.

Kilio cha barabara katika Jimbo la Ukonga chini ya Rais Samia linakwenda kupata ufumbuzi na tayari wakandarasi wamepatikana na ujenzi utaanza wakati wowote kuanzia sasa.

Silaa ameongeza kuwa Ukonga hivi sasa ujenzi wa barabara ya mwendo Kasi awamu ya Tatu inaendelea kujengwa.”Rais Samia hatuna tunachomdai ila yeye ndio anatudai.

Barabara ya kuanzia Banana mpaka Kitunda iko Jimbo la Segerea na inaurefu wa kilometa tano na zitajengwa.Wenyeviti hawa tumewataka watembee kifua mbele na wanayopasiwedi ambayo ndio CCM .”

Related Posts