Kamata aomba ridhaa kwa Wananchi nafasi ya Mwenyekiti “Maji na Barabara na Simama navyo”

Wakati zoezi la Kampeni likiendelea nchini kote, Mgombea wa nafasi ya Uwenyekiti Mtaa wa Kigoto Kata ya Buhongwa wilaya ya Nyamagana Jijini Mwanza Godfrey Kamata, kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM amewaahidi wananchi wake kuwa endapo watampa ridhaa basi maji na Barabara ndio kipaumbele chake.

 

Kwa upande wake Diwani wa kata hiyo Benard Kabadi ametumia nafasi hiyo kumuombea kura kwa Wananchi huku akiahidi mashirikiano ili kutatua na kuleta maendeleo kwenye mtaa huo.

 

Zimesalia siku mbili zoezi la kupiga kura kufanyika ambapo November 27, 2024, Wananchi watachagua Wenyeviti wa Mtaa, Kijiji na Kitongoji.

 

Related Posts