Group) limejiunga na watoa huduma wa teknolojia ili kutengeneza fursa kwa
vijana barani humo kupitia ujuzi wa kidijitali kama sehemu ya ahadi yake ya
kukuza ujuzi wa kidijitali kwa kizazi kijacho cha Afrika. Kwa kushirikiana na (Amazon
Web Services) AWS, Microsoft, Skillsoft na mashirika mengine, Vodacom inalenga
kufungua fursa za ajira kwa vijana milioni moja ifikapo mwaka 2027 kwa
kuboresha ujuzi wa kidijitali katika nchi nane za Afrika.
Vodacom Digital Skills Hub
itapatikana katika nchi za Afrika Kusini, Ethiopia, Tanzania, Msumbiji,
Lesotho, Misri (Talimy), Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (VodaEduc) na Kenya
(Industry Digital Talent Program) ili kuwapa nguvu vijana katika kuzalisha
wabunifu wa kidijitali wa baadaye, na kuwezesha jamii ya kidijitali ya Afrika
huku ikitumia mifumo ya kujisomea mwenyewe (u-learning) iliyopo katika masoko
husika.
Kulingana na Shirika la
Kimataifa la Fedha (IFC), zaidi ya ajira 230 milioni zitahitaji ujuzi wa
kidijitali barani Afrika ifikapo mwaka 2030, ambapo kwa wakati huu bara hili
linakutana na pengo kubwa kati ya upatikanaji wa ujuzi wa kidijitali na
mahitaji ya ujuzi huo.
“Mataifa mengi ya Afrika
yanakutana na changamoto kubwa za ukosefu wa ajira, ukosefu wa usawa wa
kijinsia, tofauti za kipato na upatikanaji mdogo wa elimu, huduma za afya na
huduma muhimu. Changamoto hizi zinachochea dhamira yetu na kuongoza mkakati
wetu wa kuungana kwa ajili ya mustakabali bora, tukitumia teknolojia za
kidijitali kuleta usawa kwa ajili ya kuboresha maisha ya watu. Uzinduzi wa
Vodacom Digital Skills Hub ni uthibitisho wa dhamira yetu ya kuwa vinara katika
njia ya kuunda Afrika ya kidijitali na yenye usawa,” alisema Shameel
Joosub, Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Group.
Vodacom Digital Skills Hub
itatoa mafunzo ya ujuzi wa kidijitali yaliyothibitishwa na mamlaka husika huku
mtu akijifunza kwa kasi yake binafsi kwa vijana kati ya umri wa miaka 18 na 35.
Hii ni pamoja na majukwaa ya e-learning yaliyopo tayari katika masoko ya
Vodacom kwenye nchi husika.
Madarasa ya mtandaoni na
e-learning yamewezesha wanafunzi katika maeneo ya mbali au yasiyohudumiwa
kufikia elimu bora kupitia majukwaa kama Talimy nchini Misri, e-Fahamu nchini
Tanzania, VodaEduc nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Faz Crescer
nchini Msumbiji na jukwaa la e-learning nchini Afrika Kusini, likitoa
rasilimali nyingi mtandaoni zinazokidhi mahitaji mbalimbali ya kujifunzia.
“Kama kampuni inayozingatia
dhamira ya kuunganisha vijana kwa ajili ya mustakabali bora, tunafurahia mpango
huu unaolenga kuhamasisha kizazi kipya cha wabunifu wa kidijitali. Lengo letu
kuu katika mpango huu sio tu kusaidia upungufu wa ujuzi wa kidijitali barani
Afrika bali pia kukuza vipaji vya vijana na hivyo kuendeleza mustakabali wa
kidijitali wa Afrika, hivyo kuongeza fursa za uwezeshaji katika uchumi wa
jumuishi wa kidijitali,” alisema Vivienne Penessis, Mkurugenzi wa
Rasilimali Watu wa Vodacom Tanzania Plc.
Vodacom Digital Skills Hub imeanzishwa
ili kuwawezesha vijana, hasa wasichana, kufikiria kazi katika sayansi,
teknolojia, uhandisi na hisabati (STEM), na inajumuisha mafunzo ya vitendo ya
ujuzi wa kidijitali kwa vijana barani Afrika. AWS Educate ni mojawapo ya
programu za kwanza zitakazotolewa kupitia Vodacom Digital Skills Hub na
kuongeza programu nyingine kwa majukwaa ya u-learning yaliyo katika nchi
mbalimbali, zikiwa na lengo la kuwawezesha vijana katika maeneo ya STEM. Nchini
Tanzania, AWS inakuja kama nyongeza kwa juhudi za kuhamasisha vijana wa
Tanzania kama vile VYB, ambayo inalenga vijana wenye umri kati ya miaka 15 hadi
28.