Wachezaji wa mpira wa vikapu wa nchini wamefurahia malipo ya bonasi ya kushinda mechi maarufu kwa jina la Locker Room Bonus yaliyoanzishwa na wadhamini wakuu wa michuano ya ligi ya kikapu ya Tanzania, chapa ya kubashiri ya betPawa.
Kupitia malipo la Locker Room Bonus, mchezaji na viongozi wanne, upokea malipo ya Sh140, 000 baada ya ushindi wa mechi. Malipo hayo ufanywa moja kwa moja kwenye akaunti zao za simu mara tu mechi inapomalizika tena kabla kuondoka uwanjani.
Katika michuano hiyo iliyomalizika wiki iliyopita, timu ya Dar City ya Dar es Salaam ilitwaa ubingwa kwa wanaume na Fox Divaz ya mkoa wa Mara zilitwaa ubingwa kwa upande wa wanawake na kila moja kuzawadiwa kitita cha Sh2.8 milioni.
Zawadi hizo ni mara ya kwanza kwa timu kushinda mashindano hayo yaliyofanyika kwenye uwanja wa Chinangali, Dodoma, kuzawadiwa zawadi nono nchini baada ya betPawa kusaini mkataba wa mwaka mmoja na shirikisho la mpira wa kikapu Tanzania, TBF.
Mbali ya zawadi hizo za washindi wa kwanza, betPawa pia iliwazawadia washindi wa pili, timu ya ABC kwa upande wa wanaume na DB Lioness kwa upande wa wanawake Sh1.4 milioni kila moja.
Mbali ya zawadi za washindi wa jumla, betPawa pia iliwazawadia wachezaji mbalimbali kwa kutambua kazi nzuri ndani ya uwanjani. Wachezaji hao ni Guibert Nijimbere wa Dar City aliyekuwa mchezaji bora kwa upande wa wanaume na Michele Fotshing Sokoudjou wa Fox Divas kwa wanawake ambao kila mmoja alipata Sh700,000.
“Lengo letu kubwa ni kuleta hamasa kwa wachezaji, timu na viongozi na ndiyo maana tukaingia ushirikiano na TBF. Kupitia zawadi ya Locker Room Bonus tulizowapa wachezaji, pia tumeawazawadia wale waliocheza kwa kiwango cha juu wakati wa mashindano,
Kupitia Locker Room Bonus, kila mchezaji na viongozi wanne wa timu iliyoshinda kila mechi iliyocheza walizawadiwa Sh140,000. Unaona jinsi gani timu , wachezaji na viongozi walivyofaidika na ushirikiano wa betPawa na TBF, ” alisema Afisa Masoko wa kanda ya Afrika Mashariki wa betPawa, Nassoro Mungaya.
Kwa upande wake, mchezaji wa Vijana Queens, Khadija Karambo alisema kuwa amefuraishwa sana na malipo ya Locker Room Bonus na kumfanya kuongeza bidii zaidi.
“Hii ni mara ya kwanza katika historia kuona kifurushi cha udhamini kinachonufaisha moja kwa moja wachezaji. Hizi ni juhudi ambazo kweli zimetufanya tupigane kwa bidii zaidi kushinda,” alisema Karambo.
Mbali ya Tanzania, betPawa imeanzisha zawadi hiyo katika nchi nyingi za Afrika na michezo mbalimbali.
Nchi hizo ni Shirikisho la mpira wa miguu la Uganda (FUFA Drum, Futsal), Shirikisho la Vyama vya Mpira wa Kikapu la Uganda (FUBA), na Shirikisho la mpira wa miguu la Ghana.
“Programu hii imeifanya ligi kuwa na ushindani zaidi, ikiongeza hamasa kwa timu kutoa kiwango cha juu zaidi. Wachezaji sasa wanajua kuwa kuna kitu cha kupigania, hata kama hawashindi ubingwa, kila ushindi wa mchezo unawapa sehemu ya zawadi inayosaidia kufidia mahitaji yao,” alisema Nahodha wa timu ya JKT Stars, Jescal Julius Ngisase.
Kwa upande wake, kocha wa Fox Divas, Barick Martin Kilimba, alisema Zawadi ya Locker Room Bonus imetimiza ndoto ya muda mrefu kwa wachezaji wa mpira wa kikapu.
“Uwazi na msaada kwa kupitia betPawa umeleta furaha kubwa kwa wachezaji na makocha. betPawa imeongeza ushindani, ikiwahamasisha wachezaji kuboresha mchezo wao na kushindana kwa kiwango cha juu zaidi. Udhamini huu umeleta maendeleo na msisimko mkubwa ndani ya ligi,” alisema Kilimba.
Orodha ya zawadi kwa washindi ipo hivi:
-Bingwa wa Wanaume: Dar City- Sh 2,800,000
-Mshindi wa pili kwa Wanaume, ABC- Sh 1,400,000
-Mshindi wa tatu kwa Wanaume, UDSM Outsiders – Sh700, 000
-Bingwa wa Wanawake, Fox Divas – Sh2, 800,000
-Mshindi wa pili kwa Wanawake, Don Bosco Lionesses – Sh1, 400,000
-Mshindi wa tatu kwa Wanawake, JKT Stars – Sh 700,000
-MVP wa Wanaume, Guibert Nijimbere wa Dar City – Sh 700,000
-Mfungaji bora kwa Wanaume, J’shin Brownlee wa Dar City – Sh420,000
-Mlinzi bora kwa Wanaume, Elias Nshishi wa ABC – Sh280,000
-Mchezaji bora Chipukizi kwa wanaume, Yekonia Mpambaje wa ABC-Sh 280,000
-MVP wa Wanawake, Michele Sokoudjou wa Fox Divas – Sh700,000
-Mfungaji bora kwa Wanawake, Michele Sokoudjou wa Fox Divas – Sh420,000
-Mlinzi bora kwa Wanawake, Taudensia Oloch wa DB Lioness – Sh280,000
-Mchezaji Bora chipukizi kwa Wanawake, Asia Naata wa Orkeeswa – Sh 280,000