Wagombea wote mliochaguliwa msijiondoe, Serikali imezingatia Demokrasia kwa kila mgombea :Dkt Biteko

Naibu waziri Mkuu na Mjumbe wa Kamati kuu ya Halmashauri Kuu Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa , Dkt. Dotto Biteko amewataka viongozi wa vyama mbalimbali vya kisiasa waliopitishwa Majina yao kugombea nafasi mbalimbali za Uongozi ngazi ya Serikali za Mitaa kutojiondoa kwani Serikali imezingatia Demokrasia kwa kila mgombea pamoja na chama chake.

Kauri hiyo ameitoa wakati akiwanadi Viongozi wagombea katika Mkutano uliofanyika katika uwanja wa Shule ya Uwanja Mara Baada ya kupata taarifa za Baadhi ya wagombea kutoka vyama mbalimbali kujiondoa na kutoshiriki katika Uchaguzi unaotarajia kufanyika Novemba 27.

” Leo Geita tunayoizungumza Maendeleo yako kila kona tunataka mtuletee viongozi watakao ungana na Madiwani wetu madiwani watakao ungana na mbunge wetu mbunge atakaye peleka shida kwa mh rais matatizo ya watu wa Geita yaondoke msituletee kiongozi ambaye hajui hata anachotaka kukifanya , ” Dkt. Biteko.

” Nimeambiwa hapa eti kuna wengine wameamua kujitoa hata kama wamejitoa watapigwa au watabaki ndani watapigwa kwa sababu fomu walijaza wenyewe na nawaomba msijitoe baking twende hadi mwisho huu mziki wa mwaka huu chini ya Dkt.Samia Suluhu Hassan tunataka kuleta heshima kwenye nchi yetu kwamba hii nchi ni ya Kidemokrasia , ” Dkt. Biteko.

” Hatutaki vyama vya Upinzani viminywe wala hatutaki mtu yoyote anyanyaswe tunataka kila mmoja aende akafanye kazi na ushindi ndugu zanguni watu wa Geita ni kujipanga ngoja niwambie mipango ilivyo hata wenzetu tupime mipango tuliyonayo kwenye mkoa wetu wa Geita ukiangalia kwenye maeneo yetu yaliyowekwa wagombea wao wanaweka wagombea mijini hawana shida na kura za watu wa vijijini , ” Dkt. Biteko.

Related Posts