Walimu mkoani Singida wapewa pongezi kwa kazi nzuri

Mkuu wa Mkoa wa Singida Halima Dendego amewapongeza walimu wa mkoa wa Singida kwa kazi nzuri wanayoifanya kila siku na hiyo inawafanya wazidi kutoa wanafunzi wanaofanya vizuri.

Ameyasema hayo jana tarehe  katika tamasha la walimu ambalo wameliita Walimu na Samia lililofanyika viwanja vya bombadia Mkoani Singida lililojumuisha walimu zaidi ya 2000.

Dendego amewataka walimu wazidi kuwafundisha wanafunzi kwa jitiahada ili elimu izidi kukua.

“Mimi nafurahishwa sana na kazi zenu mnazozifanya ndio maana mkiniita nakuja endeleeni kufanyakazi kwa bidii ili watoto wetu wapate elimu bora,” Dendego

Naye Mwenyekiti wachama cha Walimu mkoa wa singida amefurahishwa na uwepo kwa juhudi zinazofanywa na Rais Samia kwa kutatua baadhi ya changamoto zao kama walimu.

“Ni kweli tunachagamoto ila baadhi yake zimetatuliwa na uongozi wa Samia hivyo tunaendelea kujitahdi ili kuboresha zaidi, madaraja mseleleko yametufikia tunashukuru,”

Related Posts