WANA MTWARA WAMPONGEZA RAIS SAMIA KUBORESHA BANDARI MTWARA

Na Mwandishi wetu

Wananchi wa Mtwara wamempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuleta fedha zilizopelekea maboresho makubwa ya Bandari ya Mtwara.

Rais Samia ametoa fedha zilizopelekea Bandari kupanuliwa na ununuzi wa mitambo.

“Leo hii tunaona meli kubwa kubwa zikiingia Bandari ya Mtwara, tunaona mitambo mikubwa ya upakiaji na ushushaji wa mizigo ni kazi kubwa ya Rais Samia aliyotufanyia Wana Mtwara.” Alisema Said mkazi wa Bandari.

“Sisi wana Mtwara tunajivunia Rais Samia kwani ametukomboa Wana Mtwara asitokee Mtu akajitapa eti amefanya yeye ama bila ya yeye Bandari isingeboreshwa. Amefanya kwa fedha zake? Yeye ndio ameidhinisha fedha za utekelezaji? Iweje ajitape? Sisi wana Mtwara tunajua kazi ya maboresho ya Bandari fedha imeidhinishwa na Rais Samia na yeye ndio anaetoa maelekezo ya utekelezaji wa maboresho “. Alisema Hajra mkazi wa Chikongola.

Rais Samia hivi karibuni alitoa kauli Korosho isafirishwe Bandarini na akahakikisha anapeleka vifaa vipya vikiwemo kreni mbili za rununu, mashine kushughulikia makasha matupu “reach stackers” na Tag Boats za kisasa. Wana Mtwara wanasema Ahsante sana Rais Samia.

 

Related Posts