HIFADHI za Taifa Tanzania Wameandaa safari ya kuupanda Mlima Kilimanjaro tarehe 9 Disemba 2024 katika maadhimisho ya miaka 63 ya uhuru wa Tanganyika ambapo wamekuja na kauli mbiu ya: “Stawisha Uoto wa Asili Tanzania, Okoa barafu ya Mlima Kilimanjaro”.
Huu ni msimu wa nne wa kampeni ya Twenzetu Kileleni, tayari kampeni imezinduliwa rasmi itaenda mpaka Disemba 4, 2024, hivyo wadau mbalimbali wanakaribishwa kushiriki ikiwemo kuchangamkia kujisajili na kulipia.
Msimu huu njia tatu zitakazotumika katika kupanda Mlima Kilimanjaro ni ya Marangu, Machame na Lemosho.
Kwa njia ya Marangu, Kampuni ya ZARA ADVENTURE TANZANIA wameweka gharama nafuu zaidi ili kila Mtanzania apate nafasi kwa kiasi cha Tsh. 1,550,000 ambayo itajumlisha: Kupanda, Chakula, Kulala, Mavazi ya kupandia Mlima, na mambo yote muhimu.
“Karibuni sana na tuendelee kushirikiana ili jambo letu liwe kubwa na kubwa zaidi mwaka huu.
Kwa maulizo na usajili tafadhali tuwasiliane kwa namba maalum ya Twenzetu Kileleni kwa kutuma ujumbe WhatsApp number hii 0653811138 ,
#twenzetukileleni2024
#twenzetuuhurupeak2024