BATA LA DISEMBA KUKUTANISHA WATU ZAID 1000, BURUDANI NA BIA

 

Zaidi ya Watu elfu Moja wanatarajiwa kujitokeza katika Tamasha la Bata la Disemba linalotarajiwa kufanyika Disemba 6 hadi 8 2024 katika Viwanja vya Leaders Jijini Dar es salaam.

Ameyabainisha hayo Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Albert Chalamila wakati akizungumza na Waandishi wa Habari hu Kwa lengo la kuuhabarisha Umma kuhusu Tamasha hilo lenye lengo la Kampuni ya Heinikeni kutoa fursa ya kulinuanjua Jiji kuwa kitovu cha kiutamaduni Sanaa na biashara.

Chalamila amesema wakati Jiji likiebdelea kusukuma ukuaji wa uchumi Nchini matukio kama hayo yanaonyesha uwezo wa kuvutia Wawekezaji wa Kimataifa na Utalii na kuinua uchumi unaostawi.

Aidha Mkuu wa Mkoa amewaomba watu wote kujitokeza viwanja vya leaders club  ili waweze kuwa sehemu ya watu watako burudika kwenye bata la Disemba.

Ameongeza kuwa Tamasha hilo  litawavutia watu wengi wakiwemo  wageni kutoka kanda zote  za mkoa  wa Dar es salaam na nje ya mkoa wa Dar es salaam.

“Furahia wewe na familia yako kuelekea kufunga mwaka na kutakuwa na michezo ya watoto, wapishi wa nishati safi, chakula bora, viwanji na lengo  lazima tukupeleke kwenye furaha isiyokuwa na ukomo” amesema Albert chalamila

Kwa Upande wake Meneja Masoko kutoka katika Kampuni ya Heinikeni beverages Lilian Pascal amesema katika Tamasha hilo kitakuwepo mambobalimbali ikiwemo burudani,chakula,vinywaji,na kukuza Vipaji na kuinua uchumi ikiwa ni katika kuelekea kuadhimisha miaka 63 ya uhuru wa Nchi.

“Nao wanamitindo watapata  fursa ya kuonyesha bunifu zao kwani kanivi inatarajiwa  kuwa sehemu kuu ya watengeneza  mtindo  na  washawishi” amesema 

Pia tamsha hilo litaambatana na burudani kutoka kwenye kwa wasanii  mbalimbali wa muziki wa bonge kutoka nchuni Tanzania

Related Posts