NLD YAHITIMISHA KAMPENI KWA KISHINDO HANDENI,YAWAOMBA WANANCHI KUWAPA RIDHAA WAGOMBEA WAO ILI WAWAPE MAENDELEO

 


Na Oscar Assenga,HANDENI.

CHAMA cha The National League For Democracy (NLD) kimehitimisha kampeni kwa wagombea ambao wanawania nafasi za uongozi katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 27 mwaka huu huku wakiwawataka wananchi kuwapa ridhaa ili waweze kuwapa maendeleo.

Akizungumza wakati wa mkutano wa kampeni wa kuhitimisha kampeni hizo katika viwanja vya soko la Misima wilayani Handeni,Katibu Mkuu wa NLD Doyo Hassani Doyo alisema kwamba chama hicho kimejipanga kuhakikisha wanatatua kero za wananchi zinazowakabili kwa muda mrefu.

Alisema kwamba wagombea ambao wamewasimamisha kwenye maeneo yote wanauwezo mkubwa wa kuweza kuwatumikia wananchi na kuwasaidia kutatua changamoto ambazo zinawakabili kutokana na kwamba wanatosha na uwezo wa kuwaongoza.

“Sisi katika uchaguzi huu tumewasimamisha wagombea wasiokuwa na njaa lakini pia wenye uwezo wa kutoa ajira kwa wengine kupitia fursa tulizonazo na wengi wametoa ajira kwenye jamii zinazowazunguka”Alisema

Awali akizungumza Mwenyekiti wa NLD wilaya ya Handeni Rajabu Doyo aliitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa kufanya uchunguzi haraka iwezekanavyo kwa baadhi ya wagombea wa vyama vya siasa kuandika barua za kujitoa kwenye uchaguzi huo wa Serikali za Mitaa.

“Haiwezekani mgombea anachukua fomu ya kugombea anaijaza halafu akairudisha alafu leo unaambiwa kajitoa hii ni rushwa ya wazi wazi kabisa kwa hiyo tunaiomba Takukuru iingilie kati haraka iwezekanavyo “Alisema

Related Posts