Xavi amtaja fowadi wa Azam

KOCHA Mohammed Mrishona Mohammed ‘Xavi’ ambaye anawafundisha mazoezi binafsi wachezaji mbalimbali wa Ligi Kuu Bara, Championship na wanaocheza nje amemzungumzia mshambuliaji wa Azam FC, Nassor Saadun namna anavyotakiwa kufanya zoezi la umaliziaji na utulivu anapofika golini.

Saadun ni kati ya wachezaji ambao wanafundishwa na kocha huyo, alisema mchezaji huyo yupo fiti, ana uwezo wa kupambana na beki akibakia mmoja, isipokuwa zoezi analotakiwa kulifanyia kazi kwa nguvu zote ni umaliziaji.

“Japokuwa mabadiliko ya makocha Azam yanaweza yakambadilisha aina ya uchezaji wake, hilo siyo ishu kikubwa kwake angalau aweze kutumia nafasi kwa kadri awezavyo,” alisema Shavi ambaye ni kocha wa wa timu ya taifa ya vijana ya Zanzibar chini ya umri wa miaka 15 na alikuwepo benchi Stars ikishinda bao 1-0 dhidi ya Guinea.

“Ukiachana na Saadun nimewafundisha wachezaji mbalimbali kama Feisal Salum ‘Fei Toto’, Abdallah Shaibu ‘Ninja’, Hassan Kessy,  Crispin Ngushi, kina Abdi Banda, Simon Msuva huwa wanakuja kufanya mazoezi, wachezaji wapo wengi, lakini kila mmoja inalingana na kile alichokifanya alikotoka, pia wanaocheza Ligi ya Wanawake.

“Mchezaji bila mazoezi binafsi hawezi kufiti kila kitu kupitia mazoezi ya timu, nilikuwa mchezaji najua hilo, hivyo lazima wajitume ili kile wanachokitarajia kukifanya watimize kwa wepesi.”

Related Posts