Beki Mlandege afichua siri | Mwanaspoti

BEKI wa Mlandege, Mohamed Daud ‘Dume’ amesema siri ya ushindi wao dhidi ya KMKM ni kucheza kwa kufuata maelekezo ya kocha.

Mlandege FC waliibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya KMKM katika mchezo wa Ligi ya Kuu ya PBZ uliochezwa Novemba 24 mwaka huu kwenye Uwanja wa Mao A, Unguja.

Baada ya ushindi huo Mlandege FC imepanda mpaka nafasi ya kwanza katika msimamo ikiwa na alama 24 huku KMKM SC ikishuka hadi nafasi ya nane na pointi zake 17.

Dume alisema mchezo ulikuwa mgumu kutokana na ubora wa wapizani wao  lakini kwa sababu kila mchezaji alifanya majukumu yake vizuri aliyopewa na mwalimu wao ndiyo maana wameibuka na ushindi.

“Malengo msimu huu ni kuwa mabingwa na ili uwe bingwa lazima ushinde mchezo, tunashukuru mpaka sasa bado hatujapoteza, tumeshinda sita na sare sita,† alisema.

Mlandege FC wana michezo mitatu ya kucheza kukamilisha mzunguko wa kwanza dhidi ya Kipanga FC utakaochezwa leo Alhamisi kwenye Uwanja wa Mao A, kisha dhidi ya New City FC na Zimamoto FC.

Related Posts