Mbunge wa Jimbo la Mchinga Mkoani Lindi Mama Salma Rashid kikwete amewaongoza wananchi wa Jimbo hilo kushiriki zoezi la upigaji wa Kura kuchagua viongozi wa Serikali za mitaa, vijiji na vitongoji
Mama Salma ameshiriki zoezi hilo Katika kituo cha kupiga Kura cha Makasini kijiji cha Ruvu Kata ya Mchinga huko manispaa ya Lindi
Akizungumza mara baada ya kupiga Kura mama salma kikwete amewasisitiza wananchi kuendelea kujitokeza Katika vituo vya kupigia Kura ili kutimiza wajibu wao wa kidemokrasia
Msimamizi wa Uchaguzi wa kituo hicho chama makasini Joseph Jeremiah anaeleza Hatua za Awali kwa kabla ya kushiriki kupiga Kura huku baadhi ya wananchi wakieleza namna ya zoezi hilo linavyoenda