Mchengerwa: Uchaguzi umekwenda vizuri, matokeo ya jumla kesho

Dar es Salaam. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Mohamed Mchengerwa amesema maeneo ya changamoto yaliyobainika yameongezewa muda wa saa mbili kutoka saa 10 hadi saa 12 jioni ndio walimaliza kupiga kura.

Kuhusu changamoto zilizojitokeza, Waziri Mchengerwa amesema,”yako maeneo changamoto zimejitokeza, lakini asilimia 98 hali imekwenda vizuri, hata malalamiko si mengi na yanapotokea yanatusaidia ili kusonga mbele.”

Amesema, “yako maeneo ambayo yametulazimu kuongeza muda badala ya kumaliza saa 10 jioni waliongeza saa mbili na eneo kama la Ruaha Morogoro tumesema wafanye kesho,”amesema.

Waziri Mchengerwa amesema matokeo ya jumla anatarajia kuyatoa kesho Alhamisi na maeneo mengine wameruhusu wasimamizi wa uchaguzi wanapomaliza watangazwe.

Aidha, Waziri huyo amesema uchaguzi huu umekuwa wa kihistoria ambao umezungumzwa na makundi mbalimbali na wananchi wamejitokeza kujiandikisha na kupiga kura, na kubwa Watanzania wameendelea kutunza amani.

Related Posts