Nimepiga kura nimetimiza haki yangu ya kikatiba :Kapinga

Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Judith Kapinga leo ameshiriki zoezi la kupiga

kura katika Kitongoji cha Mheza kijiji cha Mkumbi Halmashauri ya Mbinga Vijijini ili kuchagua viongozi wa eneo husika.

Kapinga ameeleza kuwa, kwa kufanya hivyo ametimiza haki yake ya kikatiba na kutoa wito kwa Watanzania wote kuitumia haki hiyo kikamilifu.

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ni miongoni mwa mihimili muhimu ya Demokrasia inayowezesha ushiriki wa wananchi katika uongozi wa maeneo yao.

 

Related Posts