Dar es Salaam. Rais Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za pole kutokana na kifo cha Dk Faustine Ndugulile, Mbunge wa Kigamboni na Mkurugenzi Mteule wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Kanda ya Afrika.
Dk Ndugulile amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Jumatano, Novemba 27, 2024 nchini India alipokuwa akipatiwa matibabu.
“Nimepokea kwa masikitiko taarifa ya kifo cha Dk Faustine Ndugulile, Mbunge wa Kigamboni na Mkurugenzi Mteule wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Kanda ya Afrika, kilichotokea usiku wa kuamkia leo Novemba 27, 2024.”
“Ninatoa salamu za pole kwa familia, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dk Tulia Ackson, wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wananchi wa Kigamboni, ndugu, jamaa, marafiki na Watanzania wote.” Ameandika Rais Samia
Dk Ndugulile alikuwa Mkurugenzi mteule wa Shirika la Afya Dunia Kanda ya Afrika (WHO) ambaye alipaswa kuanza majukumu hayo mapya Februari 2025.
Endelea kufuatilia Mwananchi.