SHEIKH NA MUFTI WA TANZANIA DKT ABUBAR ZUBER AMEPIGA KURA HUKO KOROGWE

 


Shekh na Mufti Mkuu wa Tanzania Dkt Abubakar Zuber  ametekeleza haki yake ya msingi  kupiga kura katika Mtaa wa Mndolwa alikojiandikosha huko Mkoani Tanga katika Wilaya ya Korogwe

Akizungumza mara baada ya zoezi hilo Mufti amesema anashukuru Mwenyezi Mungu amesafiri kutoka Jijini Dar es salaam hadi kufika Tanga akiambatana na Waandishi wa habari na kupokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Korogwe kuweza kutimiza wajibu ambao ni haki ya Msingi.ya kila raia wa Kitanzania.kuitekeleza kuchagua viongozi watakaowafaa kwa kipindi cha miaka mitano kwa  kuwaletea maendeleo

Kwa Upande wake Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Willium Mwakilema amesema anashukuru wanananchi wote wanaendelea kujitokeza kupiga kura katika vituo mbalimbali na mpaka sasa ametembelea vituo vyote asubuhi maandalizi ni ya kutosha na hali ni shwari

Aidha amesema uchaguzi huo ni muendelezo wa Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika 2025 kuchagua Wabunge, Madiwani na Rais hivyo ni vyema wananchi kuendelea kudumisha hali ya amani na Utulivu hadi watakapojipatia viongozi wanaowataka waepukane na rushwa

Related Posts