VIONGOZI WA INEC WASHIRIKI UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2024

 

Mwenyekiti Wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Mhe.Jaji (Rufaa) Jacobs Mwambegele, akipiga kura katika kituo cha Shule ya Sekondari Jamhuri kililichopo Halmashari ya Jiji la Ilala Mkoani Dar es Salaam leo. Wananchi wanapiga kura leo katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa.


Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Bw. Kailima Ramadhani akipiga kura katika Kituo cha mtaa wa Chimuli II kilichopo Shule ya Msingi Chadulu jijini Dodoma leo.


Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Mhe. Jaji Asina Omari akipiga kura katika kituo cha Serikali ya Mtaa Masaki iliyopo Halmashari ya Wilaya ya Kinondoni Mkoani Dar es Salaam leo. Wananchi wanapiga kura leo katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Mhe. Balozi Omar Ramadhani Mapuri akipiga kura katika kituo cha Serikali ya Mtaa Ali Hassan Mwinyi , kilichopo – Mikocheni Halmashari ya Wilaya ya Kinondoni Mkoani Dar es Salaam leo. Wananchi wanapiga kura leo katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa.


Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Mhe. Magdalena Rwebangira akipiga kura katika kituo cha KIJICO , kilichopo – Kijitonyama Halmashari ya Wilaya ya Kinondoni Mkoani Dar es Salaam leo. Wananchi wanapiga kura leo katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

Related Posts