Wadau wapongeza BOT kwa kudhibiti wanaokiuka taratibu za kifedha

Benki ya biashara ya Mkombozi leo Novemba 25,2024 imezindua huduma yake mpya ya wakala wa kimkakati Ili kuwa karibu zaidi ya na wateja wake.

Akizungumza kabla ya uzinduzi huo, Padre Dennis Wigira Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Yosefu Jimbo kuu Katoliki la Dar es salaam ambaye alimuwakilisha Askofu Mkuu wa Jimbo Hilo Mhashamu Jude Thaddeus Ruwa’ichi katika hafla hiyo amesema anaamini katika weledi wa wahudumu wa benki hiyo na kuwasihi kuongeza juhudi kufikia wateja mbali mbali.

“Watu wanapenda Watendaji waaminifu, wateja wanapenda huduma zinazofuata taratibu za kibenki na hivi katika kutunza weledi huo tuwe na Hofu na Mwenyezi Mungu juu ya huduma za kibenki kwa njia ya Mkato na hizo njia za mkato ndio zilizo angusha Taasisi za fedha au zimepoteza sifa nzuri na mbaya zaidi kama kanisa linapoteza sifa nzuri katika huduma za kifedha”.

Pia wamewashukuru mamlaka inayosimamaia bank (BOT) kwa kuweza kutoa idhini kwa mabank kutoa huduma za mawakala, kwani huduma hii inasaidia katika kukuza uchumi kwa kuifikia jamii kwa urahisi.

Related Posts