CPL MWIKWABE AKABIDHI KITI MWENDO KWA MTOTO MWENYE ULEMAVU WA KUZALIWA

Polisi kata ya Ikoma Tarafa ya Grumet Wilayani Serengeti Mkoani mara CPL Emmanuel Mwikwabe amekabidhi kiti mwendo kwa mtoto Vaileth Enock(16) mwenye ulemavu wa kuzaliwa ambao umepelekea kupooza.

CPL Emanuel Mwikwabe alimbaini Mtoto huyo kupitia kampeni ya utoaji wa Elimu ya polisi jamii Nyumba kwa Nyumba katika Kijiji cha parknyigoti kitongoji cha Park B kupitia Baba yake mzazi Mzee Enonck Komanya.

“nilifanikiwa kufika nyumbani kwa Mzee Enonck Komanya nakuwakuta watoto miongoni mwa watoto nilio wakuta kwenye mji huo ni pamoja na Binti huyu Vaileth na ndipo nikaamua nimshirikishe Mkuu wa Wilaya Bi.kemirembe na kukubali kunishika Mkono kwa kunipa kiti mwendo”Alisema CPL Emanuel Mwikwabe.

Pia amesema nimekabidhi kiti hicho nakupeleka Faraja kwa Mtoto huyo ambaye toka azaliwe amekuwa akiishi kwa kulala kutokana na kukosa kiti mwendo.

Emmanuel amewataka Wazazi pamoja na wakazi katika kata hiyo kuacha kuwabagua watoto wenye ulemavu waliopo kwenye maeneo yao kwani kufanya hivyo nikuwafanyia ukatili

Related Posts