Millen Magese kuwaongoza Jokate, Idriss, Faraja na Kadinda Samia festival

Ni mwendelezo wa tamasha la Samia Fashion Festival ambayo this time anatarajiwa kwenda kufanyika Zanzibar Jumamosi hii ya Tarehe 30 huku chief judge wa Swamy hii akitarajiwa kuwa Millen Magese ambaye amekuwa akiishi Marekani

Katika mkutano na waandishi wa Habari Leo hii muandaaji wa tamasha hilo Khadija Mwanamboka aliyeambatana na Mchekeshaji Idris Slutani amesema kuwa ni kipindi cha Mapinduzi Katika tasnia ya fashion na Urembo ambapo Zanzibar kutakuwa na majaji wengi akiwemo Jokate Mwegelo, Idriss Slutani, Faraja Nyalandu na Martin Kadinda ambao wote wataongozwa na chief Judge Millen Magese huku wakiwa na dhamira ya uundaji wa Vazi la Samia ambalo linabeba Alama ya Stars, Uongozi na Heshima.

Kwa upande wa Millen Magese amesema kuwa amekuwa “Kwa zaidi ya miaka 20 nimejitolea Maisha yangu katika sekta ya Mitindo, niliposikia kuhusu mpango huu sikusita nilipanda Ndege kuja Nyumbani kuwa sehemu ya historia” Millen

Kwa Upande wa Idriss amemuomba Rais Samia kuruhusu Madereva na wataendaji wa Serikali kuvaa Vazi la Samia kama vile ambayo wamekuwa wakilivaa Vazi la Kaunda Suit..

 

 

Related Posts