RAIS SAMIA ATUNUKU KAMISHENI KWA MAAFISA WANAFUNZI 236


Na Pamela Mollel,Arusha

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Samia Suluhu Hassan,ametunuku kamisheni kwa Maafisa Wanafunzi 236 cheo cha luteni Usu,kwa kundi la 05/21-shahada ya Sayansi ya kijeshi(BMS)na kundi la 71/23-Regular katika chuo cha Mafunzo ya kijeshi Monduli leo tarehe 28 Novemba 2024

Aidha kati ya wahitumu hao wanaume 196 na wanawake 40

Maafisa hao wapya wamekuwa Maafisa wa jeshi la Ulinzi la wananchi wa Tanzania (JWTZ)Katika cheo cha Luteni Usu ambapo kundi la 05/21-BMS lenye idadi ya 75 wamepata mafunzo kwa muda wa miaka mitatu na kuhitimu shahada ya Sayansi ya kijeshi

Aidha kundi la 71/23-Regular lenye idadi ya 95 Maafisa wapya wamepata mafunzo yao kwa muda wa mwaka mmoja na Maafisa wengine wapya 88 wamepata mafunzo yao kutoka nchi rafiki za Afrika na nje ya Bara la Afrika

Hata hivyo Kabla ya kutunuku kamisheni Mhe. Rais na Amiri Jeshi Mkuu alikagua gwaride lililoandaliwa na Maafisa Wanafunzi kutokana na maelekezo ya Mkuu wa chuo cha Mafunzo ya kijeshi Monduli,Meja Jenerali Jackson Jairos Mwaseba na kusimamiwa na Kaimu mkufunzi Mkuu Kanali Ally Mohamed Ninga na Kisha kutoa zawadi kwa Maafisa Wanafunzi waliofanya vizuri

Baada ya kamisheni Mhe, Rais alitunuku shahada ya Sayansi ya kijeshi kwa Maafisa wapya 75 pamoja na kuvunja mahafali hayo

Akizungumza katika mahafali hayo ya tano ya shahada ya kwanza Sayansi ya kijeshi,Mkuu wa chuo cha Mafunzo ya kijeshi Monduli Meja Jenerali Jackson Jairos Mwaseba anasema chuo hicho kinaona fahari kubwa kwani hii ni mara ya pili kuwezesha mafunzo ya shahada hiyo kwa kujisimamia pasipo na ushirikiano wa kimafunzo na chuo cha Uhasibu Arusha

Sherehe za kamisheni na mahafali zimehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali na kijeshi.

Matukio mbalimbali wakati wa sherehe za kutunuku Kamisheni kwa Maafisa Wanafunzi 236 wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania katika sherehe zilizofanyika katika Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi (TMA) Monduli mkoani Arusha tarehe 28 Novemba, 2024

 

Related Posts