15 wafariki dunia, zaidi ya 100 hawajulikani walipo maporomoko ya udongo

Dar es Salaam. Watu 15 wamefariki dunia na wengine zaidi ya 100 hawajulikani walipo baada ya maporomoko ya udongo yaliyosababishwa na mvua kuharibu makazi katika vijiji kadhaa mashariki mwa Uganda, wilayani Bulambuli jana Novemba 28, 2024.

“Kuna vifo vya watu 15 na tuna hofu kuwa bado kuna miili mingine mingi iliyofunikwa,” amesema Charles Odongtho, ambaye ni msemaji wa Ofisi ya Waziri Mkuu inayosimamia majanga.

Kaya 40 zimefunikwa kabisa na nyingine kuharibiwa. Miundombinu kama madaraja na barabara imeharibiwa, ikizuia juhudi za uokoaji kutokana na eneo hilo kutofikika.

Polisi wamesema kuwa watu 113 bado hawajapatikana ambapo mvua kubwa tangu Oktoba imekuwa ikisababisha mafuriko na maporomoko katika maeneo mbalimbali nchini humo.

Endelea kufuatilia Mwananchi.

Related Posts