Alichokisema Dk Nawanda baada ya kuachiwa huru

Mwanza. Muda mfupi baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Mwanza kumuachia huru aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Dk Yahya Nawanda, mwanasiasa huyo ametoa kauli yake kuhusiana na uamuzi huo.

“Namshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema, naishukuru familia yangu, naishukuru mahakama imetenda haki, namshukuru kaka yangu Alex kwa kazi kubwa ambayo ameifanya, basi Mungu ni mwema, kila kitu kinatoka kwa Mungu, utukufu unatoka kwa Mungu,” amesema Dk Nawanda.

Katika uamuzi wa kesi ya kulawiti iliyokuwa inamkiabiri, Hakimu Mkazi Mfawidhi Erick Marley amesema Mahakama imefikia uamuzi huo kwa kuzingatia mambo matatu –kukosekana kwa ushahidi wa kisayansi, maelezo ya mashahidi kutoshabihiana na uchunguzi wa daktari kutothibitisha iwapo ni kweli manii za mshtakiwa huyo zimekutwa sehemu za siri za mshtakiwa huyo.

Katika uamuzi huo, Hakimu Marley amesema mahakama hiyo baada ya kupitia maelezo ya ushahidi na vielelezo imejiridhisha kuwa hakukuwa na muunganiko wa ushahidi unaoweza kumtia mshtakiwa hatiani na hivyo imemwachia huru.

Related Posts