Aliyekuwa RC Simiyu aachiwa huru

Mwanza. Mahakama ya Hakimu Mkazi Mwanza imemuachia huru aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Dk Yahya Nawanda katika kesi ya kulawiti iliyokuwa ikimkabili.

Katika uamuzi wake kwenye kesi hiyo ya jinai namba 1883/2024, yenye kosa la kulawiti, uliosomwa na Hakimu, Mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo Erick Marley.

Katika uamuzi huo, Hakimu Marley amesema mahakama hiyo baada ya kupitia maelezo ya ushahidi na vielelezo imejiridhisha kuwa hakukuwa na muunganiko wa ushahidi unaoweza kumtia mshtakiwa Dk Nawanda hatiani na hivyo kumwachia huru.

Endelea kufuatilia Mwananchi

Related Posts