MADEREVA WAHIMIZWA KUZINGATIA TIJA KATIKA UTENDAJI KAZI

 

Na Mwandishi wetu – Dar es salaam

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Zuhura Yunus, amewahimiza Madereva kuzingatia tija na ufanisi katika utendaji kazi  ili kuhakikisha jamii inafanya kazi  za kiuchumi kwa usalama, kukuza uchumi  wao na uchumi wa  Taifa kwa ujumla

Ameyasema hayo leo Novemba 28, 2024 wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya ustadi wa kuboresha Tija na Ufanisi kwa madereva jijini Dar es Salaam. 

“Changamoto ya ajali barabarani zinaathiri nguvu kazi ya Taifa na kupunguza pato, hivyo basi ni muhimu kuzingatia mafunzo haya ili kupunguza ajali ambazo zinaweza kuepukika” amesema

Awali akizungumza Mkurugenzi wa Ukuzaji Tija, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Yohana Madadi, amesema lengo la Mafunzo hayo ni kutoa ujuzi na mbinu za udereva bora ili kupunguza ajali barabarani na kutii sheria bila shuruti.

 

Related Posts