Mahakama yamuachia huru Nawanda – Millard Ayo

Mahakama ya Hakimu Mkazi Mwanza imemuachia huru aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Dkt. Yahya Nawanda aliyekuwa akikabiliwa na kesi ya kulawiti.

Katika uamuzi wake kwenye kesi hiyo ya jinai namba 1883/2024 uliosomwa na Hakimu Mkazi Mfawidhi Erick Marley, Mahakama hiyo baada ya kupitia maelezo ya ushahidi na vielelezo imejiridhisha kuwa hakukuwa na muunganiko wa ushahidi unaoweza kumtia Dkt. Nawanda hatiani na hivyo imetangaza kumuachia huru kuanzia sasa.

 

Related Posts