MMILIKI WA GOROFA LA KARIAKOO LILILOUWA WATU HIVI KARIBUNI AFIKISHWA MAHAKAMANI.

 

 

Na Karama Kenyunko Michuzi Tv 

MMILIKI wa Gorofa la Kariakoo lililoanguka hivi karibuni na kupelekea vifo vya watu 31 na kuacha wengine majeruhi Leondela Mdete na wenzake wawili, wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka 31 ya kuua bila kukusudia.

Mbali na Mdete, washtakiwa wengine ni Zenabu Islam 61) na Ashour Awadh Ashou (38) 

Katika hati ya mashtaka iliyosomwa mahakamani hapo na wakili wa serikali Adolf Lema akisaidiana na Grace Mwanga na Erick Kamala imedai washtakiwa walitenda makosa hayo Novemba 16, 2024 katika mtaa wa  Mchikichi na Congo eneo la Kariakoo jijini Dar es Salaam.

Mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Godfrey Mhina inadaiwa siku ya tukio isivyo  halali, washtakiwa walishindwa kutimiza majukumu yao na kusabashisha vifo vya Said Juma, Hussein Njou, Prosper Mwasanjobe, Shadrack Mshingo, Godfrey Sanga, Neema Sanga, Elizabeth Mbaruku, Hilary Minja, Abdul Sululu, Chatherine Mbilinyi na wengine 21

Hata hivyo washtakiwa wamekana kutenda kosa hilo na mshtakiwa Mdete ameachiwa huru kwa dhamana wakati mshtakiwa Islam na Ashour wakirudishwa rumande kwa kushindwa kutimiza masharti ya dhamana ambayo yaliwataka kuwa na

wadhamini wawili kila mmoja wenye barua za utambulisho, kitambulisho cha Taifa na walitakiwa kusaini bondi ya Shilingi Milioni Tano kwa kila mmoja.

Kesi imeahirishwa hadi Desemba 12, mwaka huu 2024

Related Posts