Tabora, JKT zatakata, Yacouba wamotoo

Tabora United ikiwa kwenye Uwanja wa KMC Complex imeendeleza moto wake wa ushindi baada ya kuichapa KMC mabao 2-0.

Mbali na ushindi wa KMC, JKT Tanzania imefanikiwa kujiweka kwenye nafasi nzuri baada ya kuichapa Fountain Gate bao 1-0 kwenye Uwanja wa Kwaraa Mkoani Manyara.

Katika mchezo wa Tabora ambayo imeendelea kubaki nafasi ya tano na pointi 21 ikicheza michezo 13, mabao ya mchezo huu yalifungwa na Yacouba Songne na Offen Chicola wakiendeleza moto wao wa ushindi kwenye mechi za hivi karibuni.

Sasa KMC imeendelea kuporomoka na inashika nafasi ya kumi ikiwa na pointi 14 baada ya kucheza michezo 13.

Kwa upande wa JKT huu ni mchezo wake wa kwanza inashinda ugenini, ikiwa ilijipatia bao lake katika dakika ya 34 kupitia kwa Najimu Maguli.

Sasa JKT imesogea hadi nafasi ya nane kwenye msimamo ikiwa na pointi 16 baada ya kucheza michezo 11 tu.

Related Posts