Dar es Salaam. Wafanyabiashara watatu wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam wakikabiliwa na mashtaka 31 ya kuua bila kukusudia.
Washtakiwa hao ambao wanadaiwa kuwa wamiliki wa jengo lililoanguka mtaa wa Mchikichi na Congo, Kariakoo jijini Dar es Salaam na kusabanisha vifo vya watu 31, wamefikishwa mahakamani hapo leo Ijumaa Novemba 29, 2024 na kusomewa mashtaka hayo.
Waliofikishwa mahakamani hapo ni Leondela Mdete (49), mkazi wa Mbezi Beach, Zenabu Islam (61), mkazi wa Kariakoo na Ashour Awadh Ashour (38), mkazi wa Ilala.
Washtakiwa hao wamesomewa kesi hiyo na mawakili watatu waandamizi wa Serikali – Adolf Lema, Grace Mwanga na Erick Kamala mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Godfrey Mhini.
Kwenye mashtaka hayo, washtakiwa hao wanadaiwa Novemba 16, 2024 katika mtaa Mchikichi na Congo, Kariakoo jijini Dar es Salaam, isivyo halali, kwa pamoja walishindwa kutimiza majukumu na kusabashisha vifo vya watu 31.
Endelea kufuatilia mitandao ya kijamiia ya Mwananchi