WATU watatu ambao ni wamiliki wa jengo la Ghorofa la Kariakoo lilioporomoka tarehe 16 Novemba, 2024, wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashataka 31 likimewo mauaji bila kukusudia. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Leo tarehe 29 Novemba 2024 wakili wa serikali Adolf Lema, Grace Mwanga na Erick Kamala Mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Godfrey Mhini wamewasomea mashatka 31 watuhumiwa hao.
Watuhumiwa hapo ni pamoja na Ashour Awadh Ashour (38), Mkazi wa llala, Leondela Mdete (49), Mkazi wa Mbezi Beach na Zainab Islam (61), Mkazi wa Kariakoo .
Kwa pamoja watatu hao wanadaiwa kuwa ni Wamiliki wa jengo lililoanguka Mtaa wa Mchikichi na Congo, Kariakoo jijini Dar es Salaam na kusabanisha vifo vya Watu 29.