BARRICK NORTH MARA KIDEDEA TUZO KUBWA ZA MWAJIRI BORA 2024

Mgodi wa North North Mara uliopo wilayani Tarime mkoani Mara ambao unamilikiwa kwa ubia na kampuni ya Barrick na serikali ya Tanzania kupitia kampuni ya Twiga minerals kwa mara nyingine tena imeshinda tuzo kubwa ya jumla ya mwajiri bora inayotolewa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE).

Tuzo nyingine ambazo mgodi huo imeshinda ni Uwajibikaji kwa Jamii, Afya na Usalama Mahali pa kazi, Mshindi wa pili katika kipengele cha Mwajiri Bora sekta binafsi, na uzingatiaji wa kanuni za Maudhui ya ndani Mgodi wa Barrick Bulyanhulu nao umeshinda katika kipengele cha uzingatiaji wa sheria na kanuni kutoka Mamlaka za usimamizi.

Hafla ya kukabidhiwa tuzo hizo imefanyika Novemba 29 2024 katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam ambapo Mgeni rasmi alikuwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Dotto Biteko.

Akiongelea mafanikio ya mgodi wa North Mara, Meneja Uhusiano wa Barrick, Georgia Mutagayhwa, amesema ushindi wa tuzo hizo unadhihirisha mgodi huo unavyoendeshwa kwa weredi na viwango vya kimataifa ukitoa kipaumbele kikubwa katika suala la uzingatiaji afya na usalama sambamba na ukuzaji wa vipaji vya Watanzania.

“Migodi yote ya Barrick inaongozwa na Watanzania na asilimia 96% ya wafanyakazi ni wazawa. Pia kampuni Imekuwa na mpango wa kuwezesha wafanyakazi Wanawake ambapo kwa sasa wanafanya kazi kwa ufanisi katika vitengo mbalimbali.

“Suala la kudumisha uhusiano mzuri na Wafanyakazi linapewa umuhimu mkubwa sambamba na kuendesha programu za kuwajengea afya nje kwa kushiriki mazoezi na michezo mbalimbali.

Migodi ya Barrick na Twiga pia imekuwa mstari wa mbele kuunga mkono jitihada za Serikali kutekeleza miradi ya kuleta mabadiliko chanya katika jamii za maeneo yanayozunguka migodi yake hususani katika sekta za elimu, Afya, Maji safi na salama na ujenzi wa miundombinu ya barabara.Kati ya mwaka 2020 hadi 2024 Barrick North Mara imewekeza zaidi ya shilingi bilioni 22 katika kutekeleza miradi 253 ya kijamii.
Show trimmed content


Related Posts