TCAA YANYAKUA TUZO 3 KATIKA TUZO ZA MWAJIRI BORA 2024

Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA), imenyakua tuzo tatu katika usiku wa utoaji wa tuzo za Mwajiri Bora zilizofanyika jijini Dar es Salaam Novemba 29, 2024.

Katika usiku huo wa tuzo TCAA imenyakua tuzox ya Mshindi wa Kwanza wa Maudhui ya Ndani, Tuzo ya mshindi wa pili ya Mwajiri Bora katika Sekta za Umma na Tuzo ya jumla ya Mwajiri na Mtendaji Bora.

Tuzo hizo zimekabidhiwa na Naibu Waziri Mkuu Dkt. Doto Biteko aliyekuwa Mgeni rasmi, akiambatana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu Mhe. Ridhiwani Jakaya Kikwete

Tuzo hizo huandaliwa kila mwaka na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) lengo likiwa ni kushindanisha taasisi mbalimbali katika nyanja za usimamizi bora wa rasilimali watu mahala pa kazi.

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko akimkabidhi Mkurugenzi wa Idara ya Udhibiti Uchumi katika Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA), Daniel Malanga cheti cha udhamini kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) wakati wa hafla ya kutoa tuzo za waajiri bora kwa mwaka 2024 zinazoratibwa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) ziliyofanyika Novemba 29, 2024 jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu Mhe. Ridhiwani Jakaya Kikwete akimkabidhi tuzo Mkurugenzi wa Idara ya Udhibiti Uchumi katika Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA), Daniel Malanga wakati wa hafla ya kutoa tuzo za waajiri bora kwa mwaka 2024 zinazoratibwa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) ziliyofanyika Novemba 29, 2024 jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Idara ya Udhibiti Uchumi katika Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA), Daniel Malanga akionesha tuzo katika sekta ya umma kwa mwaka 2024 wakati wa hafla ya kutoa tuzo za waajiri bora kwa mwaka 2024 zinazoratibwa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) ziliyofanyika Novemba 29, 2024 jijini Dar es Salaam.

Related Posts