Tasac yang’aa tuzo uandaaji taarifa ya hesabu kimataifa

Dar es Salaam. Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (Tasac) imeshika nafasi ya kwanza katika tuzo ya uandaaji na uwasilishaji wa taarifa za mahesabu kwa viwango vya kimataifa kwa mwaka 2023 kati ya mamlaka tisa za udhibiti zilizoshindanishwa na Bodi ya Taifa ya Uhasibu nchini.

Tuzo hiyo imetolewa na mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Benjamin Mashauri ambaye ni mkaguzi mkuu wa ndani wa Serikali.

Tuzo hiyo iliyotolewa Novemba 29, 2024 katika ukumbi wa mikutano wa APC Bunju, jijini Dar es Salaam, imepokelewa na Mkurugenzi wa Fedha, CPA Pascal Kalomba kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu  wa TASAC, Mohamed Salum.

Akizungumza katika hafla ya utoaji tuzo hiyo, Mashauri amesisitiza umuhimu wa taasisi za umma kuzingatia viwango vya kimataifa katika uandaaji wa taarifa za kifedha, ili kuboresha utawala bora.

Kwa upande wake, Kalomba amesema mafanikio hayo ni matokeo ya juhudi za pamoja za wafanyakazi wa shirika hilo.

“Hii inaonyesha dhamira yetu ya kuhakikisha kuwa rasilimali za umma zinasimamiwa kwa uwazi, uwajibikaji, na ufanisi,” amesema.

TASAC imeshika nafasi ya kwanza kwa mara ya tatu mfululizo, mara ya kwanza ikiwa ni mwaka 2021, mara pili mwaka 2022 na mara tatu kwa mwaka 2023.

Mwaka 2023, jumla ya taasisi 86 za Serikali na sekta binafsi katika maeneo wanayothibiti zimeshindishwa.

Related Posts