Ujenzi wa uwanja wa AFCON Arusha wafikia 11%

Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Gerson Msigwa amesema anaridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa Uwanja wa Michezo wa Arusha unaotarajiwa kutumika kwa ajili ya Fainali za AFCON 2027 ambao hadi sasa umefikia 11% za ujenzi.

Msigwa amesema hayo wakati alipotembelea na kukagua maendeleo ya Mradi wa ujenzi wa uwanja huo unaojengwa katika kata ya Olmoti jijini Arusha kwa saa 24 usiku na mchana.

Aidha, Msigwa mesema pamoja na kuridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa uwanja huo, hata hivyo amemtahadharisha mkandarasi huyo kuwa siku atakapochelewesha kazi ya ujenzi wa uwanja huo ndipo ugomvi wake na mkandarasi huyo utakapo kuja hata kabla Waziri wa Wizara yake Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro hajaja.

Msigwa amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha za ujenzi wa Uwanja huo wa Michezo wa Arusha unaotarajiwa kutumika kwa ajili ya Fainali za AFCON 2027 ambapo fedha za ujenzi wa Uwanja huo zimekuwa zikija kwa wakati kutoka Wizara ya Fedha.

 

Related Posts