WAZIRI wa Maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto Zanzibar Mhe. Riziki Pembe Juma ameitaka jamii kushirikiana kwa misingi ya maadili mema, kudumisha amani na utulivu Nchini katika kuondokana na kushamiri kwa vitendo vya ukatili, udhalilishaji, wizi na rushwa ili kuleta maendeleo ya haraka kwa maslahi ya Taifa na vizazi vyetu.
Ameyasema hayo Desemba 01, 2024 Jijini Dar es Salaam, Waziri Riziki Pembe Juma wakati wa sherehe ya siku ya maulid ya idara ya wanawake iliyofanyika katika ukumbi wa Masjid Akram Mbezi Beach nakubainisha kuwa kutokana na vitendo vya ukatii na uzalilishaji kushamiri kwa watoto, wananchi wanatakiwa kuwamakini sana jamii inayowazunguka ikiwemo hata ndugu,jamii na marafiki zao.
“tujipambeni na utamaduni huu wa kuamrishana mema na kukatazana mabaya ili nchi yetu na Taifa letu liondokane na mabaya ikiwemo rushwa, wizi, vitendo vya ukatili na udhalilishaji hasa kwa wanawake na watoto na mengineyo yaliyokatazwa na dini zetu”. amesema Waziri Riziki
Aidha, tuendelee kudumisha amani na utulivu tulionao na kushikamana kuwa kitu kimoja ili tuweze kuendelea kuijenga nchi yetu na kuleta maendeleo ya haraka kwa maslahi ya Taifa na vizazi vyetu.
“Wanawake wenzangu tuzidi kushikamana na kujiendeleza kielimu na kiuchumi sambamba na kusimamia wajibu wa kuilea jamii yetu katika misingi na maadili mema, kama tujuavyo kuwa mwanamke ndio jamii na kuimarika kwa mwanamke ndio kuimarika kwa jamii”. amesema Waziri Riziki
Hivyo, niwaombe wananchi wenzangu kuendelea kuwaombea dua na kuwaunga mkono viongozi wetu wa nchi mama yetu Dkt. Samia Suluhu Hassan na Dkt. Hussein Ali Mwinyi ili wazidi kuendelea kutuongoza katika hali ya amani umoja na usawa, na Taifa letu lizidi kubaki katika amani siku zote.
Kwa upande wake, Makamu Mwenyekiti wa Idara ya wanawake ya Masjid Akram, Zainab Asman Kasoro amesema wanaipongeza serikali na wadau mbalimbali ikiwemo Chombo cha habari cha Michuzi kwa kuwa wameendelea kushirikiana kila wakati mpaka leo tunatimiza miaka 20.
Matukio mbalimbali ya picha