Jenerali Mkunda awavisha nishani Majenerali, Maafisa kwa niaba ya Rais

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Wananchi wa Tanzania Jenerali Jacob John Mkunda kwa niaba ya Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt Samia Suluhu Hassan amewavisha nishani mbalimbali Majenerali, Maafisa na Askari wa JWTZ jijini Arusha tarehe 02 Disemba 2024.

Nishani hizo ni pamoja na Nishani ya Kumbukumbu ya Muungano Daraja la Nne, Nishani ya Utumishi Uliotukuka, Nishani ya Utumishi Mrefu, Nishani ya Utumishi Mrefu na Tabia Njema, na Nishani ya Miaka 60 ya JWTZ.

Aidha,Jenerali Mkunda amewavisha nishani ya Jumuiya ya SADC Maafisa na Askari walioshiriki Ulinzi wa Amani nchini Msumbiji chini ya mwavuli wa Jumuiya hiyo.

Akizungumza na Wanajeshi Kanda ya Arusha, Jenerali Mkunda amemshukuru Mheshimiwa Rais kwa kuwatunuku Nishani hizo.

Aidha, amewataka Wanajeshi kote Nchini Kuviishi Viapo Vyao walivyoapa, kufanya kazi kwa Nguvu zote kwa Uhodari, Uaminifu, Utii na Nidhamu ili kuweza kuilinda Nchi, kulinda Katiba na Kumtii Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu.

Related Posts