Maandalizi Mkutano wa (EAMJA) Yakamilika kwa Asilimia Mia Moja Huku Nchi ya Uganda Ikiongoza Kwa ushiriki Mkubwa.

Na Jane Edward, Arusha 

Maandalizi ya Mkutano wa 21 wa Chama cha Majaji na mahakimu (EAMJA)kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki yamekamilika kwa asilimia mia moja,huku wageni kutoka nchi wanachama wa jumuiya ya Afrika Mashariki wakiendelea kuwasili huku nchi ya Uganda ikiongoza kwa uwakilishi wa zaidi ya majaji na mahakimu mia moja.
Akizungumza na Waandishi wa habari Jijini Arusha  katika Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki(IJC),Rais wa chama cha Majaji na Mahakimu Tanzania(JMAT)Mheshimiwa John Rugalema Kahyonza amesema Washiriki wa mkutano huo wameanza kuwasili kwaajili ya kuhudhuria mkutano huo.
”Tunategemea kupokea majaji na mahakimu kutoka Uganda 116,Wakenya 81,Rwanda 48,Zanzibar washiriki 34,Majaji ambao wako EAC watashiriki 12,Wawakilishi wa Burundi watatu”Alisema
Amesema kwa mara ya kwanza mkutano huo utakuwa mkubwa na kwamba mpaka sasa hakuna changamoto yeyote .
Aidha miongoni mwa mada ambazo zitajadiliwa ni uboreshaji wa mifumo kwaajili ya utendaji haki,kukuza uchumi, sanjari na kukuza mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. 
 Hata hivyo Mkutano huo Mkuu wa 21  (EAMJA) unatarajiwa kuanza  kufanyika jijini Arusha siku ya kesho na Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Rais Dr,Samia Suluhu Hassan.

 

Related Posts