Sakata la kuwahamisha watu Ngorongoro, Samia aunda tume – DW – 02.12.2024

Wazee wa kimila wa jamii ya Kimasai, wameelezea kikao chao na Rais na kusema kwamba uamuzi wa rais umeonyesha unyenyekevu huku wakitaka uwazi na ushirikishi zaidi wa tume hizo. 

Rais Samia amefanya mazungumzo na wazee wa kimila wa jamii ya kabila la wamasai, Laigwanan mkoani Arusha.

Ameahidi kuunda tume mbili kwa ajili ya kuchunguza zoezi la kuwahamisha wakazi wa eneo hilo kutoka wilaya ya Ngorongoro Kwenda wilaya ya Msomera Tanga.

Samia amesema tume ya kwanza ni ile itakayoangalia masuala ya ardhi katika eneo hilo na tume ya pili itakuwa huru, itakayoangalia suala zima la kuhama Ngorongoro, itakayohusisha watu wachache watakaofanya utafiti na kutoa majibu.

Soma pia: TLS yakosoa kile kinachoendelea dhidi ya Wamaasai walioko Ngorongoro

Serikali inatekeleza mpango wa kuwahamisha kwa hiyari, takribani wakazi zaidi ya laki moja wa eneo la Ngorongoro, ikieleza kuwa sababu ya kuwaondoa ni kuokoa maisha ya wakazi hao dhidi ya hataria za Wanyama wakali na kulinda uoto wa asili katika eneo hilo la kitalii na kihistoria.

Tanzania Arusha | Maasai katika hifadhi ya Ngorongoro
Serikali inatekeleza mpango wa kuwahamisha kwa hiyari, takribani wakazi zaidi ya laki moja wa eneo la Ngorongoro,Picha: Huax Hongli/Xinhua/IMAGO

Hata hivyo hatua hiyo imekosolewa vikali na jumuiya ya kimataifa na baadhi ya wakazi wa eneo hilo wakisema ni hatua za kuminya haki zao.

DW, imezungumza na Mzee wa Kimila, au Laigwanan mkazi wa eneo la Ngorongoro aliyeshiriki kikao pamoja na Rais Samia jana, Simon Saitoti. Saitoti  amesema kwa kuomba msamaha kuhusu Sakata hilo, rais ameonyesha unyenyekevu.

Soma pia: Tanzania yawaondoa Wamaasai katika maeneo ya utalii

Hifadhi ya Ngorongoro, NCAA ni moja ya vyanzo vikubwa vya mapato ya utalii nchini Tanzania. Mwaka 2023, watalii 843,473 walitembelea eneo hilo, wakiwemo watalii wa kigeni 515,961, na kuzalisha Sh. Bilioni 195.

Akizungumzia hatua ya Rais kuunda tume, mmoja wa wakazi wa Ngorongoro Kijiji cha Kayakus, Kasale Mwaana,ambaye amekataa kuhama kwa hiyari akidai haki ya kuishi eneo hilo, amesema hatua ya Rais ni muhimu.

Hifadhi ya Ngorongoro ilianzishwa mwaka 1959 na serikali ya kikoloni baada ya watu wa kabila la Maasai kuhamishwa kutoka hifadhi ya Serengeti.

Soma pia: Ripoti: HRW yailaumu Tanzania kwa kuikuka haki za Wamaasai

Hata hivyo, baada ya Ngorongoro kuwa hifadhi mseto ya wanyama na binadamu kwa muda mrefu, kumekuwapo na mipango ya kuwahamisha wakazi waishio kwenye hifadh hiyo.

Related Posts