Dar es Salaam. Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amemteua Balozi Dk Mpoki Ulisubisya kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI).
Taarifa ya uteuzi wa Dk Mpoki imetolewa leo Jumatatu Desemba 2, 2024 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Sharifa Nyanga.
Vilevile katika taarifa hiyo, Joyce Mapunjo ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF).
Mapunjo anachukua nafasi ya Mhandisi Musa Iyombe ambaye amemaliza muda wake.