TPA YATWAA TUZO YA MWAJIRI BORA WA MWAKA KWENYE SEKTA YA UMMA

Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imetwaa kwa mara ya tatu mfululizo Tuzo ya Mwajiri bora wa mwaka kwenye Sekta ya Umma katika halfa ya Usiku wa Tuzo kwa Mwajiri bora kwa mwaka 2024, uliofanyika mwishoni mwa Juma Jijiji Dar es Salaam.

Katika utoaji huo wa Tuzo ambapo Mgeni Rasmi alikuwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Biteko aliyemwakilisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Phillip Mpango.

TPA Imetwaa jumla ya Tuzo Tano ambazo ni Tuzo ya mshindi wa kwanza Mwajiri bora wa mwaka kwenye Sekta ya Umma, Tuzo ya Mwajiri Bora Mzawa (Local Employer Award) mshindi wa kwanza, tuzo ya mshindi wa pili wa Jumla sekta zote (2nd Runners -up award), tuzo ya wanaofanya vizuri zaidi ( Club of best perfomers), tuzo ya mwanachama wa ATE kwa muda mrefu kwa Taasisi za Umma wa mwaka 2024 na tuzo ya Mwajiri bora wa Ndani ya Nchi.

Tuzo hizi hufanyika kila mwaka na Kuandaliwa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) kwa ajili ya Waajiri wa Sekta za Umma na Binafsi ambao wamefanya vizuri zaidi katika mwaka husika.

Related Posts