Na Mwandishi Wetu
NAIBU Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)Tanzania Bara John Mongella amesema ushindi wa Chama Cha Mapinduzi katika uchaguzi wa serikali za mitaa uliopita hivi karibuni ni kwa sababu chama hicho kimewatumia vijana kwenda kuongea na vijana wenzao namna ambavyo serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa awamu ya sita Dkt. Samia Suluhu Hassan ilivyofanya kwenye jamii nchini.
Amesema hayo leo Novemba 30, 2024 Wilayani Kibaha Mkoani Pwani wakati akifungua mafunzo ya 13 ya Uongozi ya mapitio ya juhudi za kuleta mabadiliko ya kisasa katika nyanja za maendeleo yaliyohusisha vijana viongozi kutoka nchi sita za kusini mwa Afrika katika harakati za maendeleo yaliyofadhiliwa na Chama Cha Kikomunisti cha nchini China (CPC).
Mongela amesema kuwa vijana ni kundi lenye nguvu katika jamii na CCM imebaini hilo na kuwapa jukumu hilo la kwenda kusema yanayofanywa na serikali yao katika jamii.
Mafunzo hayo yamezinduliwa leo yatahitimishwa Desemba 08, 2024.
Mkuu wa Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere Prof Marcellina Chijoriga amewaelezea washiriki hao 120 ambao wametoka kwenye vyama rafiki Kusini mwa Afrika ambavyo ni ANC (Afrika ya Kusini), FRELIMO (Msumbiji), MPLA (Angola), SWAPO (Namibia), ZANU- PF (Zambia) CCM wenyeji pamoja na CPC ambaye ni mfadhili mkuu.