Kikosi cha Yanga SC chenye wachezaji 25, kimeondoka Dar es Salaam mchana wa leo Desemba 3, 2024 kuelekea Algeria kwa ajili ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya MC Alger.
Mchezo huo wa Kundi A, unatarajiwa kuchezwa Jumamosi Desemba 7, 2024 kwenye Uwanja wa 5 July 1962 uliopo Mji wa Algiers nchini Algeria, saa 4 usiku kwa majira ya Afrika Mashariki wakati Algeria ikiwa saa 2 usiku.
Wachezaji 25 waliosafiri ni makipa Djigui Diarra, Aboutwalib Mshery na Khomein Abubakar.
Mabeki; Bakari Mwamnyeto, Dickson Job, Ibrahim Abdullah ‘Bacca’, Kouassi Yao Attohoula, Nickson Kibabage, Kibwana Shomari na Chadrack Boka.
Viungo; Maxi Nzengeli, Pacome Zouzoua, Mudathir Yahya, Khalid Aucho, Stephane Aziz Ki, Denis Nkane, Sheikhan Khamis, Duke Abuya, Clatous Chama, Jonas Mkude na Farid Mussa.
Washambuliaji; Kennedy Musonda, Clement Mzize, Prince Dube na Jean Baleke.
Yanga itaingia uwanjani ikiwa na kumbukumbu ya kutoka kupoteza nyumbani kwa mabao 2-0 dhidi ya Al Hilal katika mchezo wa kwanza hatua ya makundi kwenye michuano hiyo.
Wakati Yanga ikipoteza mchezo wa kwanza, MC Alger ilitoka 0-0 ugenini dhidi ya TP Mazembe.