JKT yanusa ubingwa BDL | Mwanaspoti

FAINALI ya tatu ya Ligi ya kikapu Dar es Salaam (BDL) ilipigwa juzi Jumatatu kati ya JKT dhidi ya UDSM Outsiders ikibakiza mchezo mmoja tu kumjua bingwa wa mwaka 2024.

Katika mchezo huo ambao JKT ilishinda pointi 67-62 na kubakiza ushindi mmoja ili itangazwe bingwa, inailazimu pia UDSM kushinda ili kusubiri mchezo wa tano na wa mwisho kuamua bingwa.

Fainali hiyo inayopigwa kwa mtindo wa mtoano ‘best of five play off’ ilipigwa kwenye Uwanja wa Don Bosco, Oysterbay na katika michezo miwili ya nyuma wa kwanza jkt ilishinda kwa pointi 67-62, wa pili UDSM ikashinda 66-55, kabla wa tatu JKT kushinda 67-62.

JKT ilitawala mchezo huo katika robo ya tatu ikiongoza kwa pointi nyingi (30-16) na benchi la ufundi la UDSM litajilaumu kutokana na kutokuwa makini kwenye kubadilisha wachezaji na wakati mwingine walimwacha mchezaji anayeppoteza mipira kizembe.

Katika robo ya kwanza JKT iliongoza kwa pointi 17-12, ya pili 17-10 na hadi mapumziko iliongoza kwa pointi 29-27 kabla ya kuongoza tena kwenye robo mbili za mwisho ya tatu 30-16 na ya nne 12-7.

Licha ya UDSM kupoteza mchezo huo, Evance Davies anayecheza namba 1 ‘point guard’ alikuwa kivutio katika mchezo huo kutokana na asisti na kufunga.

Related Posts